Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Ummy awapa Maagizo Maafisa Maendeleo ya Jamii
Nov 27, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_49327" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kusimamia uanzishwaji na uendeshwaji wa Kamati za ulinzi wa wanawake na watoto katika mikoa na Halmashauri ambazo hazijaanzishwa ili kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia hadi ngazi ya Kata na Vijiji.

Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsi leo Jijini Dodoma, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt John Pombe Magufuli imetekeleza kwa vitendo azma ya kukomesha vitendo hivyo.

[caption id="attachment_49328" align="aligncenter" width="1000"] Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akizungumza chimbuko wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia katika uzinduzi uliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_49329" align="aligncenter" width="1000"] Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Wanawake (UN-Women) Hodan Addou akieleza mchango wa shirika hilo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.[/caption]

Waziri Ummy ameongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na asasi za Kiraia katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa Kijinsia katika maeneo yote hapa nchini.

Aidha, Mhe Ummy ameagiza kuanzishwa kwa Madawati ya Jinsia Katika Taasisi za Elimu ya Juu ili kukomesha vitendo vya rushwa ya ngono na ukatili mwingine kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa madawati ya Jinsia na Watoto katika Vituo vya Polisi yapatayo 420 yamewezesha wahanga 58,059 kuripoti aina mbalimbali za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa rika mbalimbali wakiwemo watu wazima na watoto katika matukio ya ubakaji, ulawiti, vipigo na ukeketaji.

[caption id="attachment_49330" align="aligncenter" width="1000"] Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) Anna Meela Kulaya akieleza jinsia Shirika lake linavyoshirikiana na Serikali katika kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili katika uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_49332" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za Sekondari za Mkoa wa Dodoma wakiwa katika uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.[/caption]

Akizungumzia faida za madawti hayo Waziri amesema kuwa yameongeza mwamko wa wananchi katika kujiamini na kutoa taarifa za ukatilii unapotokea kwenye maeneo yao.

Kuongeza vituo vya Mkono kwa  Mkono vya Kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa Kijinsia (One Stop Centres) kutoka vituo 10 mwaka 2017 hadi 13 mwaka 2019 ili kiwezesha utoaji wa huduma rafiki na kwa haraka  kwa wahanga. Hatua hiyo inapelekea Serikali ya Awamu ya Tano kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuendelea kutekeleza Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 2017/2018- 2021/2022 ambao unalenga kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika Jamii yetu kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Kauli mbiu ya Kampeni ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa mwaka huu ni “Kizazi chenye Usawa: Simama Dhidi ya Ubakaji” kauli mbiu hii inawapa jukumu wananchi wote kutafakari wajibu wao kama kizazi kinachoamini na kuthamini usawa wa kijinsia.

[caption id="attachment_49333" align="aligncenter" width="1000"] Msanii Barbabas Classic akitumbuiza katika uzinduzi Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_49334" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wanafunzi wa moja ya shule ya Sekondari ya Dodoma mara baada ya uzinduzi wa siku 16 za Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW)[/caption]

Kauli mbiu hii inatoa msukumo wa kuhakikisha kila mtu katika nafasi yake anapaza sauti na kuchukua hatua ya kuzuia na kutokomeza vitendo vyote vya ukatili wa kingono hasa ubakaji na matendo yote ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika nyumba na mahali pa kazi na katika taasisi mbalimbali ikiwemo shule na vyuo mbalimbali.

Aidha, Serikali inapinga vikali mila, desturi na imani zote zenye madhara kwa jamii kama ukeketaji, kukatisha watoto wa kike shule kwa ajili ya kuolewa.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake Bi Hodan Addou amesema kuwa shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa makundi yote ili kujenga jamii yenye usawa.

Pia alipongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha inakomesha vitendo hivyo kupitia mpango mkakati wake na kuahidi   kuendelea kuunga mkono juhudi hizo.

Aliongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni tatizo la kidunia linalohitaji jitihada za pamoja katika kulikomesha.

Uzinduzi wa  siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia umefanyika Jijini Dodoma  na umefanywa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na kuhudhudhuriwa na Asasi zisizo za kiserikali, viongozi wa Serikali, Mashirika ya Umma pamoja na Viongozi wa Dini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi