Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wahitimu wa Shahada Nchini Wapewa Fursa ya Kupata Mafunzo ya Ualimu wa Kiswahili BAKITA
Sep 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Anitha Jonas

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka vijana wote wa kitanzania waliohitimu Shahada katika vyuo vikuu nchini kujitokeza na kwenda Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa ajili ya kupata mafunzo yatakayowasaidia  kuwa walimu wa lugha ya Kiswahili kwa wageni kutokana na wataalamu wa lugha hiyo kusuasua kujiandikisha katika kanzi data ya wataalamu wa hiyo.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifunga mafunzo ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili yaliyoandaliwa na BAKITA kwa ajili ya kuwajengea Ustadi wataalamu ya Kiswahili ili waweze kufundisha wageni lugha ya  Kiswahili.

“Mpaka sasa nimepewa takwimu za  wataalamu  tisini na sita  wa lugha ya Kiswahili nchini  ambao ndiyo waliyojitokeza  waliyojitokeza kujiandikaisha katika kanzi Data ya waatalamu wa lugha hii,kwa kweli sijui ni kwanini watanzania wanakuwa wazito katika kuchangamkika fursa badala yake mambo yakibadilika wataanza kulalamika,kwani lengo la kanzi data hii ni kurahisisha mfumo wa kuwafikia wataalamu wa lugha hii kwa haraka pale fursa zinapo kuja,”alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika sherehe za kufunga mafunzo hayo Waziri huyo mwenye dhamana na masuala ya lugha nchini alieleza kuwa kwa sasa kuna uhitaji mkubwa wa wataalamu kwa ajili ya kufundisha lugha ya Kiswahili na tayari kuna maombi yamesha kwisha wakilishwa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Sudani Kusini, Rwanda na Afrika ya Kusini kwajili ya kupatiwa waatalamu wa lugha ya Kiswahili na wataokweda kufundisha katika nchini hizo.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji BAKITA Dkt.Selemani Sewangi alimpongeza mheshimiwa Waziri Mwakyembe na kumweleza kuwa taasisi hiyo hivi karibuni inatarajia kuanza kutoa mafunzo ya ukalimani na wanatoa wito kwa watanzania wote na wataalamu wa lugha wanaoona kuwa wanauwezo wa kuwa wakalimani wa lugha mbalimbali wafike  katika ofisi yao kwa ajili ya kupata mafunzo.

“Kwa sasa lugha ya Kiswahili siyo lugha ya Tanzania pekee bali ni lugha ya Afrika nzima na kama tafiti zinavyoonyesha ifikapo mwaka 2063 bara zima la Afrika litakuwa linaongea lugha hii vizuri hivyo ni vyema kuongeza jitihada za kutosha  kwa wataalamu wa lugha hii kwa lengo la kuikuza vyema tukiwa kama watumiaji wa kwanza wa lugha hii barani Afrika,”alisema Dkt.Sewangi.

Pamoja na hayo nae Mkufunzi wa lugha ya Kiswahili kwa Raia wa Marekani wanaokuja nchini kwa ajili ya shughuli za kujitolea Bw.Majid Mswahili alialiwataka wakufunzi hao waliyotunikiwa vyeti baada ya kumaliza masomo yao kuhakikisha wanakwenda kuifanya kazi hiyo ya kutoa elimu ya lugha ya Kiswahili kwa wageni kwa weledi ili kuonyesha umahiri wa watanzania katika lugha hiyo.

Hata hivyo nae mmoja ya wahitimu wa mafunzo hayo ya lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kufundisha wageni Bi.Janeth Ngowi aliipongeza serikali kwa jitihada zake za kupambana kuhakikisha lugha ya Kiswahili inapewa heshima ndani na nje ya nchi na pia kwa kuanzisha Kanzi Data ya Kiswahili nchini kwa hii itasaidia kutoa ajira kwani lugha hii adhimu niya kujivunia.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi