[caption id="attachment_931" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kupokea mchango kwa ajili ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Serengeti Boys kutoka kwa wadau wa michezo nchini.[/caption] [caption id="attachment_934" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harriosn Mwakyembe akipokea hundi ya Shillingi Millioni 10 leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Kampuni ya Multichoice Tanzania iliyowasilishwa kwa niaba yao na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt.Hassan Abbas.[/caption] [caption id="attachment_937" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harriosn Mwakyembe akipokea mchango wa Shillingi Millioni moja kwa ajili ya Serengeti Boys leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania Bi. Salome Kitomari.[/caption] [caption id="attachment_940" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harriosn Mwakyembe akipokea mchango wa Shillingi Millioni Moja kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) iliyowasilishwa kwa niaba yao na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo.[/caption]
Picha/Habari na Shamimu Nyaki.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amepokea jumla ya shilingi 12,000,000 kutoka kwa Kampuni ya Multi Choice, Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA TAN) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa ajili ya kuisaidia timu ya Serengeti Boys.
Dkt. Mwakyembe amezipokea fedha hizo leo Jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi cha fedha zilizochangwa na wadau mbalimbali mwishoni mwa mwezi huu.
“Nawashukuru wadau wote wanaoendelea kuichangia timu yetu ya Serengeti Boys, leo nimepokea shilingi 10,000,000 kutoka Kampuni ya Mult Choice, shilingi 1,000,000 kutoka MISA TAN pamoja na shilingi 1,000,000 kutoka TAKUKURU”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa timu imeanza mashindano hayo vizuri japokuwa wametoka bila kufungana na timu ya Taifa ya Mali ambayo ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.
Aidha, ameahidi kuwa mchezo dhidi ya Timu ya Serengeti Boys na Timu ya Angola itakayochezwa Mei 18 mwaka huu itarushwa moja kwa moja kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa MISA TAN, Salome Kitomari amesema kuwa waandishi wa habari wameamua kuisaidia timu hiyo sio kwa kutumia kalamu zao kuwatangaza katika vyombo vya habari tu bali imeamua kuwasaidia kwa kuwachangia fedha.
“Tumeamua kuichangia timu yetu ili tuwape moyo zaidi wa kufanya vizuri kwani wameonesha jitihada katika mchezo wa mpira wa miguu,” alisema Bi. Salome.