Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi alipofika Ikulu Migombani Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kufuatia kifo cha baba mzazi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakizungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofika Ikulu Migombani kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuhani msiba wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa kijijini kwao Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Giza
Mwanga
Chaguo Msingi
Ndogo
Kawaida
Kubwa