Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Awataka Wawekezaji Kufuata Sheria
Aug 29, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_10864" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu wa Raisi wa Kampuni (Uendelezaji Bibiashara) wa Kampuni ya PIRIOU ya utengenezaji na ukarabati wa meli nchini Ufaransa Bwana Michel Perrin leo Jijini Parisi Ufaransa. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Bw. Samweli Shelukindo leo Jijini Parisi Ufaransa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption]

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watu wote wenye nia ya kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini Tanzania kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Agosti 29, 2017) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais (Uendelezaji Bishara) wa kampuni ya PIRIOU, Bw. Michel Perrin.

Waziri Mkuu amekutana na Bw. Perrin jijini Paris nchini Ufaransa kupitia ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Kampuni ya PIRIOU inataka kuja nchini kuwekeza katika utengenezaji na ukarabati wa meli.

Akizungumza na muwekezaji huyo Waziri Mkuu alimshukuru kwa nia yake ya kutaka kuwekeza nchini, ambapo alimtaka afuate sheria, kanuni na taratibu za uwekezaji nchini.

“Tanzania ni sehemu nzuri ya uwekezaji kwa sababu kuna fursa nyingi. Pia ni nchi yenye amani na utulivu wa kisiasa pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo nakukaribisha sana.”

Kwa upande wake Bw. Perrin amesema ameamua kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi salama na kwamba anauhakika wa kupata soko ndani ya nchi pamoja na mataifa jiraji.

Amesema anaamini uwekezaji wake nchini Tanzania utakuwa na tija, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Serikali na pia atahakikisha anafuata sheria zote za nchi.

Pia Bw. Perrin alitumia fursa hiyo kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Balozi Samwel Shelukindo kutokana na ushirikiano anaompa kuhusu masuala ya uwekezaji nchini.

Naye Balozi Shelukindo amesema atahakikisha anaendelea kutafuta wafanyabiashara mbalimbali na kuwashawishi waje kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini

 IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU, 

JUMANNE, AGOSTI 29, 2017.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi