Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Awahakikishia Wawekezaji Mafanikio
Jul 09, 2017
Na Msemaji Mkuu

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi walio hudhuria katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani, akiwa amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na. Mwandushi Wetu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewahakikishia uwekezaji wenye tija wawekezaji watakaokuja nchini kwa kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu wa kisiasa na uchumi wenye kukua kwa kasi.

Wazir Mkuu ameyasema hayo leo alipomuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Aga Khan alipochaguliwa kuwa Imamu Mkuu wa madhehebu ya Shia Isamailia duniani

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na kuthamini shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao wa taasisi za Aga Khan zilizopo hapa nchini, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana nao.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani. Kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Shia Ismailia Amin Lakhani na (kulia) ni muwakilishi wa AKDN Resident Amin Kurji, wakati alipomwakilisha Rais Dkt. John Magufuli, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ameupongeza mtandao wa taasisi za Aga Khan kwa kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika kutoa kipaumbele cha kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Nawahakikishia kwamba uwekezaji wenu hapa nchini utakuwa na baraka  kwa sababu nchi imetulia kisiasa na uchumi wake unakua kwa kasi. Nawaomba muendelee kuwaalika wanajumuia wa  madhehebu ya Shia Ismailia popote walipo duniani waje kuwekeza nchini fursa bado zipo.”

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akipokea maandano ya maadhimisho ya miaka 60 tangu Mtukufu Agakhan alipo chaguliwa kuwa Imamu mkuu wa madhehebu ya Shia Ismailia duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee, Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika sherehe hiyo, Julai 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Madhehebu ya Shia Ismailia Tanzania, Bw. Amin Lakhani ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaowapa na kwamba ameahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kuboresha sekta mbalimbali nchini.

Amesema mtandao wa maendeleo wa Aga Khan unatoa huduma mbalimbali zikiwemo za afya, elimu, kilimo na kunaendesha miradi katika mabara ya Afrika na Asia kwa kuwapa fursa watu wenye kipato cha chini kushiriki katika uzalishaji ili kujikwamua kiuchumi.

Awali, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema aliipongeza taasisi hiyo kwa mpango wake wa  upanuzi wa hospitali na kuongeza vituo 35 vya afya kutoka 15 walivyonavyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi