Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mkuu Atembelea Sabasaba, Akabidhi Matrekta 500
Jul 05, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33325" align="aligncenter" width="1000"] Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishangilia baada ya kukata utepe ikiwa ni ishra ya kukabidhi matrekta 560 yaliyonunuliwa na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam Julai 4, 2018. Watatu kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage na kushoto ni Naibu Waziri wake, Mhandishi Stella Manyanya. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kulia ni Naibu wake, Dkt, Mary Mwanjelwa.Watatu kushoto na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es aslaam, Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/caption]

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekabidhi  matrekta 560 kwa wateja wa mwanzo katika awamu ya kwanza ya uunganishaji wa matrekta maalumu kwa ajili ya shughuli za kilimo vijijini.

Amekabidhi matrekta hayo leo (Jumatano, Juni 4, 2018) wakati akifungua Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.

Waziri Mkuu amesema uchumi wa viwanda  ni pamoja  na kilimo, hivyo  ameagiza matrekta hayo yaende vijijini kutekeleza shughuli za kilimo ili kuwaongezea tija wakulima.

Wateja wa kwanza waliokabidhiwa matrekta hayo Ursus yaliyounganishwa nchini ni Wizara ya kilimo (500), Jeshi la Magereza (50) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) (10).

Amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuboresha sekta ya kilimo ili itoe  mchango unaotegemewa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia sekta ya viwanda.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua kitabu kinachotoa muongozo na taratibu za kufuata wakati wadau mbalimbali wanapotaka kujenga viwanda kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa.

Waziri Mkuu mesema lengo la mwongozo huo ni kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau wa viwanda nchi nzima.

“Kijitabu hiki kidogo kina maelezo muhimu kuhusu taratibu za kufuata unapotaka kujenga kiwanda, kuanzia kutenga maeneo ya kuvutia uwekezaji na hata kuendesha makongamano ya biashara,”.

Kadhalika, Waziri Mkuu, amewashuru na kuwapongeza washiriki wote wakiwemo wa sekta binafsi kwa ushiriki wao. Amesema kwamba Serikali inatambua kuwa sekta binafsi ndio muhimili mkuu wa kujenga uchumi wa viwanda nchini.

Pia Waziri Mkuu amegawa tuzo kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo, ambapo Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeibuka mshindi wa jumla.

Baada ya kufungua maonesho hayo, Waziri Mkuu alitembelea mambanda mbalimbali yakiwemo ya Zanzibar, Viwanda na Biashara, Asasi, Azam, TPA na EOTF.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATANO, JULAI 4, 2018.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi