Waziri Mkuu Atatua Mgogoro wa Ardhi wa Miaka Mitatu Kinondoni
Aug 17, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete kuhusu ramani ya eneo lenye mgogoro lililoko Boko - Dovya, wilayani Kinondoni katika kikao alichokiitisha ofisini kwake Oysterbay, Dar es Salaam, Agosti 17, 2022. Mgogoro huo umedumu kwa miaka mitatu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe wakati akielezea walivyotekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu ya kuwataka watatue mgogoro wa ardhi katika eneo la Boko-Dovya wilayani Kinondoni, katika kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu Ofisini kwake Oysterbay Dar es Salaam Agosti 17, 2022. Mgogoro huo ulidumu kwa miaka mitatu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni kwenye kikao alichokiitisha Ofisini kwake Oysterbay, Dar es Salaam Agosti 17, 2022.