[caption id="attachment_35363" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).[/caption]
Na: Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amewaagiza wajumbe wa baraza la chama cha walimu Tanzania kutekeleza hoja zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Hayo ameyasema hii leo wakati wa kikao cha dhararu kilichowakutanisha wajumbe hao kujadili hoja zote zilizotolewa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) katika taarifa yake ya mwaka 2016/2017.
Waziri Mhagama alieleza kuwa ripoti ya mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) imeelezea changamoto zilizokuwepo kwenye chama hapo awali ikiwemo masuala ya mapato na matumizi ya chama, mfumo wa uongozi na uwajibikaji, mikataba iliyoingiwa na chama ya uwekezaji, suala la utozaji ada kwa wananchana na mfumo wa sera ya malipo ya fedha.
[caption id="attachment_35364" align="aligncenter" width="750"]“Wajumbe wa baraza hili mkishiriki kikamilifu katika kujadili na kufikia maamuzi ya pamoja ili kutimiza malengo ya chama na kutakuwa na utaratibu utakao saidia kuongeza uwazi na mshikamano miongoni mwa wanachama” alisisitiza Mhagama.
Aliongeza pia kwa kuyatekeleza hayo chama kitakuwa na utaratibu mzuri utakao heshimiwa na kila kiongozi wa chama na wanachama wote pamoja na namna bora ya kutunza na kutumia fedha za chama ili ziweze kutumika katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa manufaa ya wanachama wote.
Aidha, Mhe. Mhagama alitoa rai kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuangalie mifumo madhubuti ya kutunza kumbukumbu za mali, madeni, michango na idadi ya wanachama kwa kuanzishwa kanzi data “data base” itakayo kuwa inatoa taarifa sahihi.
[caption id="attachment_35366" align="aligncenter" width="750"]“Mifumo hii itaondoa malalamiko miongoni mwa wanachama kutokana na upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati, pia utaratibu huu utasaidia kuongeza uwazi na kuleta maendeleo endelevu na kutimiza dhamira ya Chama kwa ujumla” alisema Mhagama.
Kwa Upande wake Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania Bi. Leah Ulaya alisema kuwa hoja zilizotolewa na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali kupitia uchunguzi aliofanya zina manufaa sana kwa chama na hakika zitabadili mwenendo wa chama uliokuwepo awali.
“Tutahakikisha mali zote zinawanufaisha wanachama na tutafuata taratibu kwa kuanzisha mfumo ambao utakuwa thabiti na utasaidia moja kwa moja kumuonesha mwanachama ameshiriki kwa namna gani ikiwemo uchangiaji wa michango yake.” Alisema Ulaya.
[caption id="attachment_35368" align="aligncenter" width="1000"]Naye Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania Bw. Deus Seif alikubali wito wa Waziri kwa kueleza kuwa watajadili hoja zote zilizotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa kina na kuhakikisha wajumbe wote wa baraza watashiriki katika mjadala huo na kufikia maamuzi ya pamoja kwa mustakabali wa chama.