Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mchengerwa Kuunda Kamati Maalumu ya Kuandaa Mdundo wa Kitanzania
Jul 13, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Meneja wa Studio ya Wanene, Humphrey Domboka akimuonesha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe, Mohamed Mchengerwa (mwenye nguo ya kitenge) baadhi ya kazi zake anazozifanya.

 Na John Mapepele


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema anatarajia kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuratibu uzalishaji mdundo wa muziki wa kitanzania ambao utaitangaza Tanzania Duniani.  


Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 13, 2022 alipotembelea studio ya kuzalisha kazi za sanaa ya Wanene na kufanya majadiliano na wafanyakazi wa studio hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

 “Dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuwa na mdundo utakaoitambulisha nchi yetu kimataifa ili kuuza utamaduni wa nchi yetu kwenye mataifa mbalimbali duniani” amesisitiza Mhe. Mchengerwa.


Amesema Kamati hiyo maalum itaundwa na walimu wabobezi kutoka vyuo vikuu, wazalishaji wa Muziki, wanamuziki pamoja na viongozi wa kimila (machifu).

Amesema Tanzania imebahatika kuwa na utajiri wa utamaduni ambao kama utatumika vizuri kutengeneza midundo  ya miziki kama ilivyo kwa nchi mbalimbali duniani utasaidia  kuitangaza Tanzania na  kuinua  uchumi wa Tanzania.

Aidha, amewapongeza wazalishaji hao wa muziki ambapo amesema wanafanya kazi nzuri ya  kuandaa kazi bora  ambazo zina ubunifu mkubwa. 

Amesema amefurahishwa kuona wazalishaji wenye ubunifu mkubwa ambapo amesisitiza kuwa kama watashirikiana kwa pamoja na Serikali wataweza.

Kwa upande wake Meneja wa Studio ya Wanene, Humphrey Domboka amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa kuwa karibu na wadau wa wa sekta ambazo anazisimamia.


Domboka amesema endapo Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kutakuwa na mapinduzi makubwa ambapo amempongeza Mhe. Rais kwa kazi kubwa anayofanya kwenye sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi