Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mchengerwa Afanya Mazungumzo na Nguli wa Filamu wa Nigeria
Jun 14, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa akimsikiliza Msanii nguli kutoka Nigeria, Jim  Iyke. Mazungumzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dodoma yamelenga kwenye mashirikiano katika kuandaa filamu za kimkakati za pamoja baina ya Tanzania na Nigeria.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana na msanii nguli kutoka Nigeria, Jim  Iyke na kufanya mazungumzo ya mashirikiano katika kuandaa filamu za kimkakati za pamoja baina ya Tanzania na Nigeria.

 
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Juni 14, 2022 jijini Dodoma ambapo wamekubaliana  kuwa na mashirikiano  kwenye filamu za kimkakati kwa faida za pande zote mbili.


Aidha,  Mhe. Mchengerwa amesema mashirikiano hayo yataifanya Tanzania kunufaika zaidi kwa kufanya kazi na manguli wa filamu wa Nigeria ambao wana wapenzi  wengi duniani.


Waziri Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watu mbalimbali duniani kuja kuwekeza  kwenye sekta ya Sanaa na Michezo.


Ameongeza kuwa kwa sasa  tayari imeshusha kodi ya zuio katika biashara ya filamu kutoka asilimia 15 hadi 10 ili kuyapa unafuu makampuni yanayofanya filamu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi