Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Mabula Akutana na Mkurugenzi wa Taasisi ya RRI
Aug 29, 2023
Waziri Mabula Akutana na Mkurugenzi wa Taasisi ya RRI
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani, Bw. Patrick Kipalu jijini Dodoma tarehe 29 Oktoba 2023.
Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani, Bw. Patrick Kipalu.

 

Dkt Mabula amekutana na Mkurugenzi huyo anayeshughulika na Programu za Haki na Jitihada za Rasilimali Ardhi katika Bara la Afrika katika ofisi ya Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 29 Agosti, 2023.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt.  Angeline Mabula (wa kwanza kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasilimali kutoka Marekani, Patrick Kipalu (katikati) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Ardhi, Imaculata Senje jijini Dodoma tarehe 29 OKtoba, 2023. 

 

 

Mazungumzo ya viongozi hao mbali na mambo mengine, yamelenga maandalizi ya Kongamano la Nne la Kimataifa litakalofanyika jijini Arusha kuanzia 12- 15 Septemba, 2023 likiwa na agenda kuu ya upatikanaji wa hatimilki za ardhi.

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki na Rasiliamali kutoka Marekani, Patrick Kipalu jijini Dodoma tarehe 29 Oktoba, 2023.

Taasisi hiyo ya Marekani ndiyo wadhamini wa kongamano hilo linalojadili masuala mbalimbali yahusuyo masuala ya ardhi ikiwemo hati milki za ardhi.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi