Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Kamwelwe Awafukuza Kazi Mameneja Kwa Kukiuka Mkataba
Oct 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_36362" align="aligncenter" width="750"] Muonekano wa mmomonyoko wa udongo karibu na barabara ya Mafinga- Nyigo KM 74.1 katika kijiji cha Litero-Nyololo.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amewafukuza kazi na kuwataka kuondoka nchini mara moja wafanyakazi wawili wa kampuni ya China New Railway 15 Bureau Group Corporation inayojenga  barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39 kwa kiwango cha lami kwa kukiuka mkataba na kudhalilisha wafanyakazi.

Wafanyakazi hao ni Meneja mradi Pen Pong na Meneja rasilimali watu Liun Migun ambao kwa pamoja licha ya kukiuka vipengele vya mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo pia wanatuhumiwa kuwapiga na kuwafukuza kazi wafanyakazi wakitanzania kwa uonevu.

[caption id="attachment_36363" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akitoa maelekezo kwa viongozi wa wilaya ya Mufindi na TANROADS mkoa wa Iringa namna ya kudhibiti mmomonyoko wa udongo katika kijiji cha Litero-Nyololo wilayani Mufindi.[/caption] [caption id="attachment_36364" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto), akisisitiza jambo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39 muda mfupi kabla ya kumuamuru aondoke hapa nchini.(Imetolewa na Kitengo Cha Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano), (Oktoba 5, 2018).[/caption]

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Matundasi wilayani Chunya Mhandisi, Kamwelwe amesema haiwezekani Serikali ikamvumilia mkandarasi asiyezingatia mkataba na anayedhalilisha wananchi ambao ndio walipa kodi zinazotumika kumlipa na kuwaonya makandarasi wote nchini kuzingatia mikataba na kutenda haki kwa wafanyakazi wao.

Waziri Kamwelwe amesema barabara ya Chunya –Makongolosi KM 39,  ambayo ujenzi wake ulitakiwa kuanza Oktoba 30 mwaka 2017 na kukamilika Januari 2020 hadi sasa imejengwa kwa asilimia 13 badala ya 20 zilizokubaliwa katika mkataba.

Aidha amesema mkandarasi China New Railway 15 Bureau Group Corporation amekiuka mkataba kwani alitakiwa awe na mitambo75 kwaajili ya ujenzi na hadi sasa ni mitambo 34 tu inayofanyakazi, awe na wataalam saba na hadi sasa ni wataalam watatu tu wanaofanyakazi licha ya kulipwa asilimia 15 ya malipo ya awali.

“Natoa miwezi mitatu kwa kampuni hii kujirekebisha na kuzingatia mkataba kabla hatua nyingine za kisheria hazijachukuliwa,” amesema Waziri Kamwelwe.

Katika hatua nyingine Waziri Kamwelwe ametoa mwezi mmoja kwa mkandarasi China Civil Engineering Corporation (CCECC), anayejenga barabara ya Mafinga –Nyigo KM 74.1 na Nyigo –Igawa KM 63.8 kukamilisha ujenzi huo  kwa mujibu wa mkataba.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Iringa  Mhandisi Daniel Kindole amemhakikishia Waziri Kamwele kuwa ujenzi huo uko katika hatua za mwisho na utakamilika kwa wakati.

Barabara ya Mafinga –Nyigo –Igawa yenye urefu wa kilometa 137.9 ni sehemu ya barabara kuu ya TANZAM ambapo katika mkoa wa Iringa ina KM 74, Njombe KM 52 na Mbeya KM 12.

Waziri Mhandisi Kamwelwe yuko katika ziara ya kukagua miundombinu ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano katika mikoa ya nyanda za juu kusini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi