Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Jafo Amjulia Muasisi wa Muungano
Jan 04, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo leo Januari 4, 2021 amemtembelea na kumjulia hali mmoja wa waasisi wa Muungano, Mzee Hassan Omar Mzee aliyelazwa katika Kituo cha Afya cha Kibweni Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Mzee Omar ambaye alichanganya udongo wakati wa sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, amelazwa katika kituo hicho cha afya akipatiwa matibabu.

Akiwa katika kituo hicho, Dkt. Jafo aliwashukuru na kuwapongeza wataalamu wa afya katika kituo hicho kwa huduma wanazotoa kwa Mzee Omar ambaye ni miongoni mwa waasisi muhimu wa Muungano.

Alisema wataalamu hao wameonesha uzalendo mkubwa kwa kutoa huduma bora kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi na waasisi wa Muungano huu adhimu wa Zanzibar.

Pia aliwasihi waendelee na moyo wa kuwahudumia wananachi wanaofika kupata matibabu kwani kituo hicho cha afya ni muhimu kwa mustakabali wa afya.    

Waziri Jafo yupo Zanzibar kwa ziara ya kikazi akiwa ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sigsbert Kavishe, Mkurugenzi Msaidizi wa Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais – Ofisi ya Zanzibar, Bi. Shumbani Ramadhan na Mratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Zanzibar, Bw. Othman Kassim Haji.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi