[caption id="attachment_1348" align="alignnone" width="750"] Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed (kushoto) akimkabaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kulia) wakati alipomtembelea Ofisini kwake mjini Unguja.[/caption]
Na Mwandishi wetu,
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohammed ameishauri Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwekeza Zanzibar ili kuwainua kiuchumi wakulima na wavuvi visiwani humo.
Mhe. Hamad amesema Visiwa vya Zanzibar vina maeneo mengi ya uwekezaji katika kilimo na kwamba uwekezaji mkubwa unahitajika ili kuongeza tija na kukuza uchumi wa Zanzibar.
“Nawahakikishia mkianza kuwekeza katika miradi kama ya mwani, uvuvi na karafuu Benki itapata mafanikio makubwa na kuitumia Zanzibar kama mfano rejea katika utoaji wa mikopo yenye tija nchini,” alisema Mhe.Hamad.
[caption id="attachment_1349" align="alignnone" width="750"]Kwa mujibu wa Mhe. Waziri, Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye utajiri mkubwa ambapo ukifanyika uwekezaji wa kimkakati utawanufaisha wananchi wengi visiwani humo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali ilianzisha Benki hiyo ili kusaidia upatikanaji wa mikopo na kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo nchini.
Bw. Assenga ameongeza kuwa Benki inatambua fursa za uwekezaji Visiwani Zanzibar na kuahidi kuanza uwekezaji mkubwa kwa wadau wa sekta za kilimo na uvuvi ambazo ni sekta zinazopewa kipaumbele kupewa mikopo na TADB.
TADB ni taasisi ya kifedha ya serikali iliyo anzishwa kwa ajili ya kutoa mikopo ya fedha ili kuendeleza sekta ya kilimo nchini.