Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Dkt. Mabula Amkabidhi Tuzo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
Jul 04, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Munir Shemweta, ARUSHA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt Angeline Mabula amemkabidhi Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete tuzo aliyokabidhiwa wakati wa Mkutano wa tisa wa Viongozi wa Majiji uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei 2022 huko Kisumu nchini Kenya.

Tuzo aliyokabidhiwa Kikwete ni tuzo ya heshima iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa) ikiwa ni kutambua juhudi zake za kuimarisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government)

Dkt. Mabula alimkabidhi Tuzo hiyo mkoani Arusha mara baada ya halfa ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mfuko wa Wanyamapori Afrika (AWF) yaliyofanyika Julai 1, 2022 katika Kituo cha Urithi wa Utamaduni.

Waziri wa Ardhi alimueleza Rais Mstaafu Kikwete kuwa, wakati alipohudhuria mkutano wa wa tisa wa viongozi wa Majiji huko Kisumu nchini Kenya alikabidhiwa tuzo hiyo kwa niaba yake kutokana na juhudi alizozionesha wakati wa utawala wake kwenye masuala ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Kwa upande wake Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Mabula kwa kuonesha uaminifu wa kuitunza tuzo hiyo tangu alipokabidhiwa Mei mwaka huu hadi alimpomkabidhi.

Wakati wa mkutano wa majiji maarufu kama Africities uliobeba kauli mbiu ya mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063 mambo mbalimbali yalijadiliwa ikiwemo hali ya miundombinu kwenye miji na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa miji hiyo.

Mameya wa miji mbalimbali, Mawaziri wa Serikali za Mitaa walihudhuria mkutano huo kwa lengo la kutafuta suluhu ya changamoto zinazowasumbua wakazi wa miji yao kama vile mipangilio mibaya ya majengo, mitaa pamoja na changamoto za  upatikanaji wa umeme.

Majiji mengine yaliyowahi kuandaa mkutano wa aina hiyo ambao unafanyika kila baada ya miaka mitatu tangu 1998 ni jijini Abidjan, Johannersburg, Dakar Kule Senegal na Marakesh Nchini Morocco.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi