Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Dkt. Mabula Akutana na Meya wa Jiji la Busan Korea Kusini
Nov 04, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Mwandishi Wetu

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Mhe. Dkt. Angeline Mabula amekutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la  Busan Metropolitan nchini Korea Kusini, Mhe. Park Heong-Joon.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Novemba 3, 2022 , Meya wa jiji hilo ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini baada ya Seoul alionesha nia ya kuendeleza mahusiano baina ya nchi hizo mbili yaliyodumu kwa takriban miaka 30 sasa.

Aidha, Mhe. Park Heong- Joon alionesha nia ya jiji lake kuwa na program za kubadilishana uzoefu kwenye nyanja za elimu sambamba na kuwa tayari kusaidia masuala ya miundombinu. Pia Meya huyo wa Jiji la Busan Korea Kusini alionesha nia ya kuja Tanzania kutembelea mbuga za wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara mapema mwakani.

Waziri wa Ardhi, Dkt. Mabula yuko katika ziara nchini Korea Kusini ambapo mbali na mambo mengine anashiriki  mijadala kwenye maonesho ya maendeleo ya teknolojia ya taarifa za kijiografia - Smart Geospatial Expo 2022.

Mwanzoni mwa ziara yake nchini Korea Kusini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula na yule wa Ardhi  Miundombinu na Usafirishaji wa Korea Kusini, Bw. Won Hee-ryong walisaini makubaliano ya ushirikiano wa  kuimarisha sekta ya ardhi kupitia hati ya makubaliano (MOU) ya ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na menejimenti ya taarifa za kijiografia.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi