Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Waziri Bashungwa Atoa Wito Wawekezaji Kuwekeza Kwenye Viwanda vya Barakoa, Vitakasa Mikono
Apr 21, 2020
Na Msemaji Mkuu

 

[caption id="attachment_52217" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akisikiliza kwa makini maelezo ya eneo la uzalishaji kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Uzalishaji vitakasa mikono kutoka Kampuni ya Total, Bw. Umesh Ankoleker (kulia) alipokua katika ziara ya Jijini Dar es Salaam ya kutembelea viwanda vinavyozalisha barakoa na vitakasa Mikono.[/caption]

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa amebainisha kwamba Serikali imejipanga kuzalisha zaidi ya Barakoa Milioni tatu na nusu kwa mwezi ili kukidhi mahitaji ya Watanzania wote.

Ameyasema hayo leo Aprili 20, 2020 alipokua katika ziara Jijini Dar es Salaam ya kutembelea viwanda vinavyozalisha barakoa (face mask) na vitakasa mikono (hand sanitizer) ambapo kwa siku ya leo ziara hiyo imefanyika katika kiwanda cha uzalishaji cha Prestine, kiwanda cha uchapishaji cha Five stars na kiwanda cha uzalishaji mafuta na vilainishi cha Total.

Waziri Bashungwa ameeleza kwamba uzalishaji wa barakoa za kutosha kwa sasa ni muhimu sana na Serikali inahakikisha kwamba Viwanda hivi vinapata malighafi ya kutosha ili viendelee kuzalisha vizuri.

“Kiwanda cha Prestine sasa hivi kinatengeneza Barakoa 30,000 kwa siku lakini baada ya vifaa kuingia kitazalisha 50,000 kwa siku na Kiwanda cha Five Star kitazalisha barakoa 100,000 kwa siku hivyo kwa ujumla viwanda hivi vitazalisha barakoa zisizopungua 3,500,000 hii ni hatua muhimu sana,”alisema Waziri Bashungwa.

[caption id="attachment_52218" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akipata ufafanuzi kuhusu matumizi ya mashine ya cherehani katika utengenezaji wa barakoa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Uchapishaji cha Five stars, Bw. Ashik Abbas Karim (kushoto) alipokua katika ziara ya Jijini Dar es Salaam ya kutembelea viwanda vinavyozalisha Barakoa na Vitakasa Mikono.[/caption] [caption id="attachment_52219" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akisikiliza kwa makini maelezo ya eneo la uzalishaji kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa Uzalishaji vitakasa mikono kutoka Kampuni ya Total, Bw. Umesh Ankoleker (kulia) alipokua katika ziara ya Jijini Dar es Salaam ya kutembelea viwanda vinavyozalisha barakoa na vitakasa Mikono.[/caption]

 Akizungumza kuhusiana na ziara yake katika kiwanda cha Total Waziri Bashungwa ameeleza kwamba uongozi umekubali kushirikiana na Serikali katika kuzalisha vitakasa mikono na tayari maandalizi ya awali yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuangalia sehemu ambayo itatumika kwa ajili ya uzalishaji.

 

“Baada ya kuangalia Kiwanda na eneo maalumu ambalo wamelitenga kwa ajili ya uzalishaji wa vitakasa mikono, na kwa uwezo wa kiwanda hiki kwa siku kitakua na uwezo wa kutengeneza lita 6000 ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali kudhibiti ugonjwa huu.” Aliongeza Waziri Bashungwa.

 

Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa watanzania na wazalishaji wengine kujitokeza na amesisitiza kuwa Serikali itawapa ushirikiano wa kipekee.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi