Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo na Katibu Mkuu Bi.Dorothy Mwanyika na Naibu Katibu Mkuu Dkt Moses Kusiluka wakiimba wimbo wa Solidarity Forever wakati wa kikao cha Baraza hilo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula wakati wa kikao cha Baraza hilo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo Bi.Dorothy Mwanyika na Naibu Katibu Mkuu Dkt Moses Kusiluka wakiskiliza hoja mbalimbali za kikao cha Baraza hilo leo Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiimba wimbo wa Solidarity Forever leo wakati wa Kikao cha baraza hilo leo Jijini Dodoma.
Frank Mvungi- MAELEZO
Watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wameaswa kuijiepusha na Vitendo vya Rushwa ili kuendelea kuongeza tija .
Akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo leo mjini Dodoma Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe . Dkt. Anjelina Mabula amesema kuwa watumishi wa Wizara hiyo lazima watambue kuwa rushwa ni adui mkubwa wa haki.
Akifafanua Mhe. Mabula amesema kuwa matumaini waliyo nayo wananchi wengi kuhusu majukumu ya Wizara hiyo ni makubwa sana .
“Hatuwezi kutoa haki kama tunapokea rushwa hivyo naagiza kila mtumishi awe mlinzi wa mwenzake, ukimwona mtumishi mwenzako anajihusisha na vitendo hivyo ni vyema akachukua hatua ya kutoa taarifa kwa mkuu wako wa kazi ili hatua stahiki zichukuliwe” Alisisistiza Mhe. Mabula
Alibainisha kuwa ni vyema watumishi wote wakajitathmini ili kuona ni wapi tunahitaji kujipanga upya ili kukidhi matarajio ya watanzania katika huduma zinazotolewa kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Mabula alitoa wito kwa watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Usimamizi wa sekta ya Ardhi nchini.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imekuwa mstari wa mbele katika kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi ambao si waadilifu.
Katika Kikao cha Baraza hilo washiriki watapata fursa ya kupitia na kujadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2017/2018, masuala ya maadili na muelekeo wa bajeti ya mwaka 2018/2019.
Katika kufanikisha jukumu la kusimamia rasilimali ardhi Mhe. Mabula amesema kuwa watumishi wa Wizara hiyo wanaowajibu wa kutumia utaalamu walionao kuhakikisha kuwa rasilimali ardhi inawanufaisha watanzania wote.
Aliwata Makamishna wa Ardhi Katika Kanda wahakikishe kuwa wanasimamia na kuhimiza makusanyo ya Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya ardhi.
Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Arddhi linafanyika JIjini Dodoma kwa siku mbili likiwashirikisha Wakuu wa Idara, Vitengo , Makamishna wasaidizi, Wawakilishi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.