Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watoto Waishio Kwenye Mazingira Magumu Wafaidika na Bima ya Afya
Jan 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27343" align="aligncenter" width="750"] Wageni wa Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini wakiangalia moja ya mradi wa ufugaji unaofadhiliwa na Mfuko wa Abbot Tanzania katika Makao ya Taifa Dar es Salaam, katikati ni Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbot Bi. Jenna Daugherty.[/caption]

Na Anthony Ishengoma

Watoto wanaoishi katika Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini wamefaidika na huduma ya Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu yao baada ya shirika la Abbot Tanzania kuwezesha ufadhili wa huduma hiyo muhimu pamoja kuwafungulia akaunti za benki ili waweze kumudu kulipia upya wakati bima zao zinapofikia mwisho wa muda wake.

Shirika hilo limekuwa mfadhili mkuu wa Makao ya Taifa ya watoto tangu mwaka 2001 na limewezesha watoto wa kituo hicho kuhakikisha wanapata huduma mbalimbali ikiwemo ustawi wa watoto kiafya na huduma nyinginezozikiwemo za vyeti vya kuzaliwa, ujenzi wa mabweni pamoja na huduma za miundombinu ya kituo hicho.

Makao ya Taifa ya watoto wenye shida Kurasini yametembelewa na ujumbe maalum kutoka Shirika linalofadhili kituo hicho cha Abbot Tanzania ili kujionea maendeleo ya shughuli za kituo hicho zinazofadhiliwa na shirika hilo.

[caption id="attachment_27344" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya watoto wa Makao ya Taifa ya Watoto wakiimba mbele ya wageni kutoka kwa wafadhili wa Makao yao Abbot Tanzania pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_27345" align="aligncenter" width="750"] Mlezi wa Makao ya Taifa ya Watoto Bi. Beatrice Mugubilo akiongoza wageni wa Makao yake kuangalia maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Abbot Tanzania.[/caption] [caption id="attachment_27347" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Simon Panga akiongea wakati wa kukaribisha wageni waliotembelea Makao ya Taifa ya Watoto Kurasini kutoka Mfuko wa Abbot Tanzania[/caption]

Akiongea wakati wa kuwakaribisha wageni hao kituoni hapo, Kaimu  Kamishina wa Ustawi wa Jamii, Simon Panga amesema Shirika la Abbot Tanzania limekuwa likitoa ufadhili wake kwa kituo hicho tangu mwaka 2001 na kufanikiwa kuleta mageuzi makubwa kwa maendeleo ya kituo hicho.

Kamishina Panga ameongeza kuwa pamoja na ufadhili wa shirika la Abbot Tanzania, Serikali imehakikisha huduma muhimu kama vile chakula, malazi, mavazi, matibabu na elimu vinapatikana kwa watoto wote wanaoishi katika makao ya watoto Kurasini.

“Watoto huletwa katika kituo hiki kupitia Maofisa wa Ustawi wa Jamii kutoka Hamashauri zote nchini wakiwa na taarifa zilizokamilika kulingana na mazingira waliyotoka na kuanza maisha kituoni hapa kwa ufadhili wa wasamalia na wafadhili kwa kushirikiana na Serikali", alisema Kamishina Panga.,”

Kituo hicho kilianzishwa mwaka 1966 pale Wamishionari walipokianzisha kwa lengo la kulea watoto yatima. Kituo kilianza na  idadi ya watoto watatu na baadae kukabidhiwa rasmi kwa Serikali ya Tanzania mwaka 1968 na tangu wakati huo Serikali ilibadili mfumo wake na kuanza kutoa huduma ya malezi kwa watoto wote wenye shida.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi