[caption id="attachment_37716" align="aligncenter" width="900"] Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake.[/caption]
Na: Frank Mvungi- MAELEZO
Msajili wa Hazina Bw. Athumani Selemani Mbuttuka amewata Watendaji wakuu , Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Taasisi na mashirika ya umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali .
Akizungumza katika Semina ya kuwajengea uwezo Viongozi hao, Bw. Athumani amesem,a kuwa lengo la Serikali ni kuona dhamira ya kuazishwa kwa Taasisi na Mashirika ya Umma inafikiwa kwa wakati.
"Kwa mujibu wa vifungu Na.10 (2) (e) na 10 (5) vya Sheria ya Msajili wa Hazina ina mamlaka ya Kusimamia Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma hivyo, tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa Bodi na Viongozi wote wanaelewa majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu"; Alisisitiza Mbutuka.
[caption id="attachment_37717" align="aligncenter" width="900"]Akifafanua amesema kuwa Bodi na Watendaji wakuu wanapaswa kuwa makini, wabunifu na kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati ili kuhakikisha kuwa Taasisi zinajiwekea mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji zinazotokana na matumizi yasiyo ya lazima hususani safari za Bodi na viongozi zisizokuwa na manufaa kwa Taasisi husika.
Alibainisha kuwa Taasisi zinapaswa kuwa na mikakati madhubuti ya kukusanya mapato ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, sambamba na kuhakikisha kuwa matumizi yote yanafanyika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali.
"Taasisi zenye utendaji usioridhisha na zile zinazopata hasara kila mwaka, kuweni wabunifu na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji na pia kuhakikisha kuwa, hoja za ukaguzi ( CAG,IAG, TR na PPRA) na maagizo ya kamati za Bunge yawekewa mkakati thabiti na zinatekelezwa ipasavyo na kwa wakati;" Amebainisha Mbutta.
[caption id="attachment_37719" align="aligncenter" width="900"]Akizungumzia Taasisi zinazopaswa kuchangia asilimia 15 ya mapato ghafi katika mfuko mkuu wa Serikali zinatekeleza wajibu huo kwa mujibu wa sheria kila robo mwaka,Bodi inatakiwa kuhakkisha kuwa, mchango unaowasilishwa ni sahihi na unaendana na kiwango cha mapato ghafi ya Taasisi husika au shirika.
Alisema kuwa upande wa matumizi hasa katika malipo ya posho, marupurupu, na maslahi mbalimbali ya Bodi, Viongozi wa Taasisi na Watumishi yanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya Serikali.
Aliongeza kuwa malipo ya posho za nyumba, posho za simu na umeme yanapaswa kulipwa kwa watumishi wenye stahili hizo kisheria tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi ya Taasisi zinaendakinyume na utaraibu huo.
Pia aliwata Watendaji wakuu na Bodi kutofanya malipo kwa kutumia nyaraka ambazo hazijaidhinishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Ofisi ya Msajili wa Hazina inafanya kazi kwa ushirikiano ili kujenga Taasisi zinazoendana na Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ambazo ni madhubuti, Bora na endelevu kwa maslahi ya wananchi wote na Taifa kwa ujumla.
Ofisi ya Msajili wa Hazina imeratibu mafunzo hayo kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma 17 kwa lengo la kuwajengea uwezo katika utendaji wao wa kusimamia taasisi hizo ili kuongeza ufanisi.