Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watanzania Watakiwa Kuwapuuza Wanaobeza Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
Nov 17, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="900"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifungua Kongamano la Pili la Kitaaluma lililoandaliwa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Mjini Dodoma mapema leo, kuhusu Fursa zilizopo Mkoani humo katika kuanzisha viwanda Vidogo na vya kati ili kuchochea ukuaji wa uchumi na dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda.[/caption] [caption id="" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akitoa maelezo kuhusu hatua iliyofikiwa katika kutekeleza dhana ya ujenzi wa Uchumi wa Viwanda na mchango wa Viwanda katika ukuaji wa uchumi endelevu hapa nchini.[/caption]

Frank Mvungi - MAELEZO, Dodoma

Serikali imewataka Wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuchochea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla kwa kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuwekeza  katika viwanda hasa vidogo na vya kati kwani ndio msingi wa kuwepo kwa viwanda vikubwa .

Akifungua kongamano la Pili la Kitaaluma kuhusu fursa zilizopo Mkoani Dodoma katika Sekta ya Viwanda Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Dodoma ina taswira mpya inayoakisi Tanzania mpya kwa maendeleo ya Taifa hivyo wanachi wajitokeze kuwekeza katika sekta   ya viwanda mkoani humo.

[caption id="" align="aligncenter" width="800"] Mkuu wa Chuo cha CBE Prof. Emmanuel Mjema akieleza sababu zilizosukuma Chuo chake kupitia Kampasi ya Dodoma kufanya utafiti kuhusu Fursa zilizopo Mkoani Dodoma hasa katika kuanzisha viwanda Vidogo na vya Kati ili kuchochea ukuaji wa uchumi na dhana ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda kufuatia hatua ya Serikali ya kuhamia Dodoma.[/caption] [caption id="" align="aligncenter" width="800"] Sehemu ya Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo.[/caption]

"Nakipongeza Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kazi kubwa za mafunzo, tafiti na ushauri wa kitaalamu mnazofanya zenye tija katika ustawi wa Taifa na hasa utafiti wenu kuhusu fursa zilizopo Mkoani Dodoma baada ya Serikali Kuhamia Dodoma," alisisitiza Mhe. Mhagama

Mhagama amesema, CBE ni Taasisi ya kwanza ya Elimu ya Juu nchini kufanya kongamano la Kitaaluma lenye lengo la Kubainisha fursa za uwekezaji kufuatia  ujio wa  Makao Makuu ya Serikali Mkoani Dodoma hivyo kuwa Taasisi ya mfano inayoendana na vipaumbele vya Serikali  ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Aliongeza kuwa sekta ya viwanda vidogo na biashara ndogo nchini ni muhimu katika kuzalisha ajira, kukuza  kipato na kuondoa umasikini ambapo sekta hiyo inaajiri  wajasiriamali  zaidi ya milioni tatu hivyo kuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

[caption id="attachment_22857" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Dodoma akitoa wito kwa wananchi wa Dodoma kutumia fursa zinazotokana na Serikali kuhamia Dodoma katika kujiletea maendeleo hasa kwa kushiriki katika ujenzi wa Viwanda.
[/caption] [caption id="" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiagana na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage mara baada ya kufungua Kongamano la Pili la Kitaaluma Mjini Dodoma mapema leo kuhusu Fursa zilizopo Mkoani Dodoma hasa katika kuanzisha viwanda vidogo na vya kati. (Picha zote na Frank Mvungi - MAELEZO, Dodoma)[/caption]

"Kulingana na sensa ya  viwanda ya mwaka 2013 iliyozinduliwa mwaka 2016 Tanzania ina jumla ya viwanda 49,243 ambapo asilimia 85.13 ni viwanda vidogo sana, asilimia 14.02 ni viwanda vidogo, asilimia 0.35 ni viwanda vya kati na asilimia 0.5 ni viwanda  vikubwa," alifafanua Mhagama.

Kwa upande Wake Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa anawapongeza wahadhiri wa chuo hicho na uongozi wake kwa kujitoa na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kujenga uchumi wa viwanda.

Aliongeza kuwa Chuo hicho kimefanya tafiti na kutoa machapisho ya tafiti hizo ndani na nje ya Chuo, hivyo ametoa rai kwa watanzania na taasisi mbalimbali kujitokeza na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kujenga  uchumi wa viwanda.

Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni "Mchango wa Viwanda Katika Ukuaji wa Uchumi Endelevu Tanzania".

Chuo cha  Elimu ya Biashara kilianzishwa tarehe 21 Januari,1965 kwa Sheria ya Bunge  Namba 31 ya mwaka 1965 kwa lengo mahususi la Serikali  kuzalisha wataalamu wa Biashara katika ngazi ya Kati.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi