[caption id="attachment_16450" align="aligncenter" width="750"] Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi Dkt. Lucas Mataba (kulia) akitoa salaam kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula wa kushoto katika maadhimisho ya makazi duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano karimjee Jijini Dar es Salaam leo wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa mipangomiji profesa John Lupala.[/caption]
Na:Paschal Dotto
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewataka wananchi kuzingatia Sheria wakati wa ujenzi wa makazi yao ili kuepuka kujenga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa jambo linalosababisha bomoa bomoa isiyo ya lazima.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Angelina Mabula aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi duniani ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Karimjee.
[caption id="attachment_16451" align="aligncenter" width="750"]Mhe.Mabula alisema kuwa ni vyema wananchi wazingatie sheria kabla hawajaanza kujenga makazi yao husika kwa kutoa taarifa kwenye ofisi husika ili kuepuka ukiukwaji wa Sheria za nchi katika ujenzi wa makazi.
“Watanzania tunakumbushwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchi kwa sababu ubomoaji unaofanyika siyo kwa makusudi bali ni kwasababu tu watu wamekiuka Sheria zilizopo na pengine watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali ambao wanawapa watu maeneo pasiporuhusiwa”, alisisitiza Mhe. Mabula
[caption id="attachment_16452" align="aligncenter" width="750"]Akizungumuzia mpango mkakati wa Wizara hiyo Mhe. Mabula alisema kuwa zaidi ya Miji 26 nchini ikiwemo Mtwara, Singida Mwanza na Dar es Salaam iko kwenye mchakato wa kupangilia makazi yake na kuwawezesha wananchi kuondokana na adha ya msongamano wa makazi.
Aidha Mhe. Mabula alisema kuwa katika maadhimisho hayo ya 32 yenye kauli mbiu isemayo ‘Sera za Nyumba :Nyumba za Gharama Nafuu’ ambayo inalenga zaidi kuimarisha sera za nyumba na makazi kwa kufuata sheria na taratibu kwa ujenzi wa makazi ya jamii yenye ubora zaidi.
Mhe.Mabula aliongeza kuwa kwa Sera hii ina madhumuni makubwa katika kuhakikisha nyumba na makazi bora yenye huduma za msingi kwa jamii toshelezi ,kuwa na mazingira salama ya kuishi kwa wananchi wote hususani wenye mahitaji maalum wakiwemo watoto, vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu pamoja na upatikanaji wa usafiri na nishati endelevu zenye gharama nafuu ,ili kuwezesha yote haya ni lazima kujua Sheria inasemaje katika kupangilia miji iliyosalama kwa manufaa ya wote.
[caption id="attachment_16454" align="aligncenter" width="750"]Alibainisha kuwa huduma nyingine ambazo zinapatikana kwenye makazi yaliyo katika mpangilio mzuri ni upatikanaji wa maji safi na salama na mfumo mzuri wa uondoshaji maji taka kwa ajili ya afya ya binadamu pamoja na uwepo wa hewa safi na ya kutosha.
“Ukienda kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kujengwa lazima wakati ukifika kwa wenyewe kulitumia watakuondoa tu kwa sababu si eneo sahihi la makazi kwa hiyo mimi niseme ili kuepuka hii bomoabomoa tusijenge bila kuwa na kibali maalumu kutoka kwenye taasisi inayohusika ili kuweza kukidhi matakwa ya sheria na taratibu za makazi salama”,alisema Mhe. Mabula.
Chimbuko rasmi la maadhimosho ya siku ya makazi duniani lilitokana na Azamio namba 40/202 la baraza kuu la umoja wa mataifa lililopitishwa Desemba,1985 na kuanza rasmi mwaka 1986.