Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watanzania Wamechoka na Michakato – Rais Magufuli
Jan 19, 2021
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Maalum - KAGERA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka kampuni ya madini ya LZ Nickel Limited ya Uingereza ianze haraka uchimbaji na uchenjuaji wa madini ya Nikeli wilayani Ngara mkoani Kagera.

“Nimefurahi pia kwa wao kuamua kujenga kiwanda cha uchenjuaji kwani ndio jibu halisi la kutoibiwa madini yetu kwa sababu madini ya nikeli yatakapochimbwa yatatoka na madini mengine, kila aina ya madini itakayouzwa, na sisi tuna mgao wetu” amesema Mheshimiwa Rais.

Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini baina ya kampuni hiyo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli amesema watanzania wamekua wakisubiri uchimbwaji wa madini hayo tangu mwaka 1976 na kwamba kwa sasa wamechoka.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amesema uwekezaji wa nchi ya Uingereza nchini ni  Dola za Marekani bilioni 5.4 na kwamba watanzania zaidi ya 277,000 wamepata ajira kwenye makampuni hayo.

“Kwa hiyo nina matumaini makubwa kwamba Kampuni hii itazalisha  ajira za watanzania, mgodi huu ukianza mapema, tutakuwa na uhakika wa ajira za watanzania milioni nane” amesema Mheshimiwa Rais.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya uchimbaji madini ya LZ Nickel Limited ya nchini Uingereza Bw. Chris Von Christianson ameunga mkono hatua ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya kuhakikisha madini yanachimbwa kwenye migodi mbalimbali na kuongezewa thamani hapahapa nchini.

“Mradi huo utakuwa wa kihistoria katika uchumi wa Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na faida yake na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji na uchenjuaji wa madini ya Nickel” amesema Bw. Christianson.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi