Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Watakaoshindwa Kufuata Muongozo wa Afya Michezoni Kuchukuliwa Hatua Kali.
Jun 10, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53107" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Waandishi wa Habari katika uwanja wa Nyamagana uliopo mkoani Mwanza[/caption]

Na Kelvin Kanje - Mwanza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, amewataka watakaoshindwa  kufuata muongozo wa afya michezoni wachukuliwe hatua kali.

Dkt. Abbasi ametoa agizo hilo jana katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo aliwaeleza wadau wa michezo kuwa Serikali imechukua uamuzi mgumu wa kufungua michezo yote  na tayari ratiba za mechi mbalimbali katika Ligi Kuu ya Soka nchini imetoka na timu zimeanza mazoezi, vilevile Serikali imetoa ruksa kwa mashabiki watakaotaka kuhudhuria  viwanjani waruhusiwe kwa taratibu maalamu.

[caption id="attachment_53109" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na uongozi wa uwanja wa CCM Kirumba, Mkoani Mwanza. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Yusuf Singo[/caption]

Akikagua utayari wa viwanja vya soka kabla ya kuanza kwa ligi, Dkt. Abbasi amesisitiza kuzingatiwa kwa Muongozo huo ikiwemo mashabiki na wachezaji kunawa kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vipukusi kabla ya kuingia viwanjani, kupimwa joto, mashabiki kukaa kwa kuachiana mita moja na kusisitiza yeyote atakayekiuka taratibu hizo atachukuliwa hatua stahiki ikiwemo viwanja husika kufungiwa kutumika kwa ligi.

“Tumefanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Katibu Tawala wake na wadau mbalimbali na wote wako tayari kuhakikisha yale yote ambayo Serikali imeagiza kwenye muongozo yanazingatiwa,” alisema Dkt. Abbas.

[caption id="attachment_53108" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na uongozi wa uwanja wa Gwambina, uliopo katika Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza nakuendelea kusisitiza umakini katika utaratibu wa kuendesha michezo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo,  Yusuf Singo.[/caption]

Katika hatua nyingine, akiwa katika wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na baadaye mkoani Shinyanga, Dkt. Abbasi amewapongeza wadau binafsi waliojenga viwanja vya Gwambina, Mwadui Complex na uwanja mwingine mpya wa Shinyanga Mjini.

“Uwekezaji huu ni mkubwa na umechangia juhudi za Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya michezo namwagiza Mkurugenzi wa Michezo awaletee wataalamu wetu ili washirikiane nanyi utaalamu katika baadhi ya maeneo hasa katika utunzaji wa nyasi za viwanja," aliagiza.

[caption id="attachment_53106" align="aligncenter" width="750"] Wachezaji wakifanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba uliopo mkoani Mwanza ikiwa ni maandalizi ya mechi zitakazofanyika katika uwanja huo hivi karibuni.[/caption]

Katika ziara hiyo Dkt. Abbasi ameambatana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Yusuf Singo na kati ya viwanja walivyovikagua ni cha CCM Kirumba na Nyamagana.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi