Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wanaovujisha Mapato Uwanja wa Taifa Kuchukuliwa Hatua Kali
Mar 15, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_51619" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na waandishi wa habari, leo Machi 15, 2020 Jijini Dodoma[/caption]

Na Mwandishi Wetu, Machi 15, 2020.

Serikali itawachukulia hatua kali  za kisheria wale wote watakaobainika kushiriki kuvujisha na upotevu wa mapato katika Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wakati wa mechi za mpira wa miguu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji  Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema, pamoja na kuongezeka kwa mapato katika mechi ya Yanga na Simba iliyochezwa hizi karibuni katika Uwanja a Taifa kufikia shilingi Milioni 545.4/=, bado  Serikali imebaini mianya ya upotevu wa mapato katika uwanja huo.

“ Serikali inawaonya wale wote waliokuwa wanashiriki katika kuvujisha na kufanikisha upotevu  wa mapato wakati wa mechi katika Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru, na kwamba haitasita kuwachukulia hatua kali dhidi yao pale watakaobainika “.

Amesema,  Serikali inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na uvujishaji na upotevu wa mapato katika viwanja hivyo ili kuziba mianya yote na tayari baadhi ya njia zinazotumika zimeshabainika.

Dkt. Abbasi amesema kwamba, kwa upande wa watendaji watakaobainika kujihusisha na uvujishaji na upotevu wa mapato, nao watachukuliwa hatua kali bila kujali nafasi zao na maeneo wanayosimamia wakati wa mechi zitakazofanyika katika viwanja hivyo.

Kutokana na kuongezeka kwa mapato ya mechi kati ya timu za Yanga na Simba , Serikali imepata mapato ya jumla ya shilingi milioni 153.2 tu. Hatua ya kudhibiti mianya ya uvujishaji na upotevu wa fedha za Serikali moja ya mikakati ya kuhakikisha kwamba Serikali inapata mapato yake sahihi kutoka katiuka vyanzo vyake. Mapato hayo ndiyo yanayoumika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kutatua kero za wananchi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi