Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Wapewa Kilomita za Mraba 2,500 Pori la Loliondo
Jun 11, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Ahmed Sagaff – MAELEZO

Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetenga eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,500 lililopo kwenye Pori Tengefu la Loliondo kwa ajili ya makazi ya wananchi.

Hayo yameelezwa leo huko Loliondo mkoani Arusha na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. John Mongella alipotembelea eneo hilo.

“Uongozi wa mkoa, uongozi wa wilaya na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama tupo Loliondo, hali ni shwari na kama mnavyojua tunaendelea na zoezi la kuweka mipaka kwenye eneo la pori tengefu la Loliondo ambalo lina kilomita za mraba 1,500.

“Na kama mtakumbuka kuwa kwa mujibu wa sheria eneo ambalo ni pori tengefu ni kilomita za mraba 4,000 lakini Serikali kwa makusudi kabisa kwa kujali shughuli za wananchi sasa imetenga kilomita za mraba 2,500 kwa ajili ya wananchi kuendelea na shughuli zao.

“Na kilomita 1,500 za mraba kwa ajili ya uhifadhi wa eneo nyeti la mazalia ya wanayama, njia zao na vyanzo vya maji, eneo hilo ndio chanzo kikuu cha maji kwenye Hifadhi ya Serengeti, Ngorngoro na Hifadhi ya Masai Mara iliyopo Kenya,” ameeleza Mkuu wa Mkoa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi