Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Waaswa Kuzingatia Utunzaji wa Mazingira Kudumisha Makazi Bora
Oct 01, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36092" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akihutubia washiriki wa maadhimisho ya siku ya makazi Duniani iliyoadhimishwa leo Jijini Dodoma. Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kauli mbiu Uthibiti wa Taka Ngumu Mijini.[/caption]  

Frank Mvungi - MAELEZO, Dodoma

Wananchi wameaswa kuzingatia usafi wa mazingira ili kuepuka athari na changamoto ya ongezezeko la taka mijini.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Makazi Duniani leo Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, amesema kuwa wananchi wanalo jukumu kubwa katika kuhakikisha suala la usafi linapewa kipaumbele na kutekelezwa kwa vitendo ili kuwa na makazi safi na salama.

“Ninatoa rai kwa wananchi waishio mijini kuzingatia utaratibu uliowekwa wa kukusanya na kutupa taka katika maeneo yaliyotengwa na kuchangia kwa hiari gharama ndgogo za uondoshaji taka na waepuke kuchimbia ama kuchoma taka katika maeneo yao ya makazi”. Alisisitiza Dkt. Mabula

Akifafanua zaidi Mhe. Dkt Mabula amesema taka ngumu zinapotenganishwa kuanzia pale zinapozalishwa hupunguza gharama za kukusanya, kuziondoa na kuziteketaza.

Kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia na kutunza mazingira Dkt. Mabula amewaasa wadau wenye uzoefu na mbinu kushirikiana na kubuni njia endelevu zisizo na athari za mazingira na zenye gharama nafuu.

Pia ameziagiza halmashauri nchini zihakikishe zinasimamia kwa ukaribu sheria ndogo za ukusanyaji taka ngumu kweeny makazi ya watu na katika sehemu zisizoweza kuleta uchafuzi wa mazingira hususan vyanzo vya maji na kutenganisha aina ya taka zitakazokusanywa na kuchakatwa kwa ajili ya matumizi mengine.

Tanzania inaungana na Jumuiya ya Kimataifa kusherehekea siku ya Makazi kupitia Azimio Namba 40/202 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Desemba mwaka 1985, ambapo maadhimisho hayo yaliadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1986 Jijini Nairobi.

Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu ya Uthibiti wa Taka Ngumu Mijini na yamefanyika Jijini Dodoma yakishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Chuo Kikuu Dodoma, Shirika la Nyumba la Taifa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

  [caption id="attachment_36093" align="alignleft" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Rose Mwanyika akifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula waakati wa maadhimisho ya siku ya makazi Duniani.[/caption] [caption id="attachment_36094" align="alignleft" width="750"] Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayeshughulikia Taaluma na Utafiti Prof. Peter Msofe akichangia mada kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa taka ngumu bila kufuata utaratibu tabia ambayo inaongeza kasi ya uharibifu wa mazingira.[/caption]   [caption id="attachment_36095" align="alignleft" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula kwenye picha ya pamoja na washiriki waliohudhuria maadhimisho ya siku ya Makazi Duniani iliyoadhimishwa leo Jijini Dodoma. Maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa Jijini Dodoma kwa kufanya usafi na kuwasilisha mada mbalimbali zinazohusu mazingira na makazi.[/caption]   [caption id="attachment_36096" align="alignleft" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akiongoza wananchi kufanya usafi katika kata ya Changombe Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yaSiku ya Makazi Duniani iliyoadhimishwa kitaifa leo jijini humo.[/caption]   [caption id="attachment_36097" align="alignleft" width="750"] Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akiweka taka katika gari la kuzolea taka mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi katika Kata ya Changombe Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho siku ya Makazi Duniani iliyoadhimishwa leo Jijini Dodoma.
(Picha na Idara ya Habari MAELEZO)[/caption]  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi