Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Waaswa Kuwafichua Wahamiaji Haramu
Dec 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi Wetu

Serikali imewaasa wananchi kutoa taarifa za kuwepo wahamiaji wanaoishi maeneo mbalimbali  nchini kinyume na sheria  za nchi ili raia wema waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na salama huku ikiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa waadilifu katika maeneo yao ya kazi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kauli mbiu ya Uhamiaji Unaozingatia Utu

[caption id="attachment_39027" align="aligncenter" width="750"] Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu..[/caption] [caption id="attachment_39028" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefamyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu[/caption]

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Naibu Waziri Masauni amesema ni lazima wananchi washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wahamiaji haramu wanaoishi maeneo mbalimbali nchini.

“Serikali ya Tanzania inaheshimu haki za kila mtu na ndio maana tumeingia mikataba mbalimbali ya kimataifa yenye kulinda utu wa kila raia awe raia au mgeni aliyepo nchini, lakini hatutokuwa tayari kuona wahamiaji wasiofuata sheria za nchi wakiingia nchini kinyume na  taratibu zilizowekwa,” alisema Masauni

"Nawasihi wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wageni wanaoingia nchini kinyume na utaratibu kwani wakiwaacha wanaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini.” Aliongeza Masauni.

[caption id="attachment_39029" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya historia ya mabadiliko ya Pasi za Kusafiria kutoka kwa mtaalamu wa pasi hizo, Sajini wa Uhamiaji, Vedasto Rweikiza(kulia), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.[/caption]

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amesema Idara yake itaendelea kutumia teknolojia katika kuendesha shughuli za uhamiaji lengo ikiwa kudhibiti uhalifu na kuiongezea mapato serikali huku akiahidi kuzuia na kudhibiti wahamiaji wanaoingia nchini kinyume na taratibu

Siku ya Maadhimisho ya Wahamaji Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Disemba 18 huku Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni “Uhamiaji Unaozingatia Utu”

[caption id="attachment_39030" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), wakiangalia pasi ya kusafiria walipotembelea mabanda ya maonyesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefamyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu.[/caption] [caption id="attachment_39031" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Dkt. Anold Kihaule, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa pasi za kusafiria, Sajini wa Uhamiaji, Vedasto Rweikiza (kulia), wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu.[/caption] [caption id="attachment_39032" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Salma Panja (kulia), baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, ambayo kwa hapa nchini yamefanyika leo, katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ikiwa Uhamiaji Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi