Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Chamwino Waaswa Kuunga Mkono Juhudi za Serikali
Feb 26, 2019
Na Msemaji Mkuu

  [caption id="attachment_40832" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Vumilia Nyamoga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Membe Wilayani humo ili waweze kutumia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo baada ya kurasimisha mashamba yao. mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo.[/caption]

Na Frank Mvungi- Dodoma

Wananchi   Wilayani  Chamwino mkoani Dodoma wameaswa kuunga mkono juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) .

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga  wakati wa kufunga mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Membe, wilayani humo yaliyoendeshwa na MKURABITA baada ya kurasimisha mashamba yao na kupata hatimilki za kimila za kumiliki ardhi ili waweze kutumia hati hizo kujiletea maendeleo.

“Fursa hii yakurasimisha mashambaiwe kichocheo cha maendeleo katika kijiji cha Membe na Wilaya yetu kwa ujumla kwa kuwa sasa mnaweza kujipatia mikopo  kutoka katika Taasisi za fedha kama mabenki baada ya kupata hati hizi za kimila la kumiliki ardhi,” alisisitiza Mhe. Nyamoga.

[caption id="attachment_40835" align="aligncenter" width="900"] Mratibu wa Mpango  wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bi Seraphia Mgembe akisisitiza umuhimu wa mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Membe Wilayani Chamwino ili waweze kutumia hati hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kujikwamua kiuchumi baada ya kurasimisha mashamba yao.[/caption]

Akifafanua, Mhe. Nyamoga amesema kuwa mashamba 1145 yamepimwa na hatimilki 1000 zimeandaliwa ili wananchi waweze kunufaika na mashamba yao baada ya kuyarasimisha na kupatiwa hati za kimila za kumilki ardhi.

Aidha, alipongeza juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo kupitia urasimishaji wa mashamba na rasilimali za wanyonge ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake mratibu wa MKURABITA, Bi Seraphia Mgembe amesema kuwa dhamira ya mpango huo ni kuwawezesha wananchi kama ilivyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza katika kuwawezesha wananchi kiuchumi ili kujenga uchumi jumuishi.

Aliongeza kuwa MKURABITA imewajengea uwezo wakulima hao ili washiriki kikamilifu katika kuzalisha kwa tija hali itakayochangia katika utekelezaji wa dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

[caption id="attachment_40833" align="aligncenter" width="900"] Kikundi cha burudani kutoka kijiji cha Membe kikitoa burudani wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa Kijiji cha Membe Wilayani Chamwino   ili waweze kutumia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi baada ya kurasimisha mashamba yao.[/caption] [caption id="attachment_40834" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Vumilia Nyamoga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wakulima zaidi ya 100 wa kijiji cha Membe Wilayani humo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima hao yakilenga kuwajengea uwezo ili waweze kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo.[/caption]

Aliongeza kuwa MKURABITA imewajengea uwezo wakulima hao ili washiriki kikamilifu katika kuzalisha kwa tija hali itakayochangia katika utekelezaji wa dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

“Natamani kuona wakulima hawa zaidi ya 100 waliopata mafunzo katika kijiji hiki cha Membe wanakuwa chachu ya mageuzi ya kiuchumi na kuwafanya wengine nao wanufaike na mafunzo hayo,”alisema Mgembe.

Kwa upande wake Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka MKURABITA, Bw. Antony Temu amesema kuwa wakulima hao wamefundishwa kilimo bora cha alizeti na mahindi,utunzaji wa kumbukumbu za mahesabu ya kilimo na biashara, uthamini ardhi na utunzaji wa mazingira, utafutaji wa fursa na kuzitumia, ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara na uandishi wa mpango wa biashara.

MKURABITA imeendesha mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima zaidi ya 100 ili waweze kutumia hati zao za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo baada ya kurasimisha mashamba yao.Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku 3 katika Kijiji cha Membe, Wilayani Chamwino.

[caption id="attachment_40831" align="aligncenter" width="900"] Wananchi wa Kijiji cha Membe wakifuatilia hotuba ya mkuu wa Wilaya ya Chamwino wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 wa kijiji hicho mwanzaoni mwa wiki yakilenga kuwajengea uwezo ili waweze kutumia hati zao za kimila kujiletea maendeleo baada ya kurasimisha mashamba yao.
                                                                     (Picha zote na Frank Mvungi)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi