Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wanafunzi 3,426 Wasajiliwa TEWW
Oct 24, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu - Dodoma

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) katika mwaka 2021/2022, imesajili jumla ya wanafunzi 3,426 katika programu tatu zilizopo katika Taasisi hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TEWW, Dkt. Michael Ng'umbi wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo Oktoba 24, 2022 jijini Dodoma kueleza mafanikio, utekelezaji na vipaumbele vya Taasisi hiyo.

Jumla ya Walimu na Wasimamizi wa elimu ya watu wazima 2,355 walihitimu masomo yao mwaka 2021/2022, alisisitiza Ng'umbi.

Aidha, Dkt. Ng'umbi amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2021/2022, TEWW ilipokea jumla ya maombi 62 kutoka kwa wadau waliomba usajili wa kuendesha vituo vya shule huria za sekondari Tanzania Bara, hata hivyo ni waombaji 58 waliokidhi vigezo na kusajiliwa.

Pia, Mwaka wa Fedha 2021/2022, TEWW ilianzisha madarasa 406 ya kimasomo ambayo yalifunguliwa katika shule za msingi za Umma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

TEWW imeendelea kutoa elimu ya sekondari nje ya mfumo rasmi na kuboresha miundombinu ya ufundishaji na ujifunzaji katika mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo jumla ya Wanafunzi 15,130 wanaendelea kupatiwa mafunzo.

Kwa upande mwingine, TEWW inatarajia kuzalisha na kusambaza nakala 3,000 za moduli za hatua II za mradi wa SEQUIP na Mihtasari nakala 2,000 kwa masomo tisa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi