Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakurugenzi wa Halmashauri za Tabora Waagizwa Kutenga Fedha kwa Ajili ya Sekta ya Ardhi
Mar 06, 2024
Wakurugenzi wa Halmashauri za Tabora Waagizwa Kutenga Fedha kwa Ajili ya Sekta ya Ardhi
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Burian akizungumza na wadau wa ardhi (hawapo pichani) kujadili namna ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika mkoa huo wakiongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Usawa Wa Kijinsia Katika Umiliki Wa Ardhi Kwa Ustawi Wa Jamii Yetu’’
Na Eleuteri Mangi, WANMM

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Burian amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri katika Wilaya za mkoa huo kutenga fedha kwa ajili ya sekta ya ardhi katika bajetiya mwaka 2024/25 ili kuendeleza utekelezaji katika maeneo yale ambayo Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) hautekelezwi.

 

Mkuu wa mkoa huo amesema wadau wa ardhi Mkoa wa Tabora wamejadili namna ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika mkoa huo wakiongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Usawa Wa Kijinsia Katika Umiliki Wa Ardhi Kwa Ustawi Wa Jamii Yetu’’

 

Akifungua mkutano huo Machi 6, 2024 mkoani Tabora, Balozi Dkt. Batilda Burian amesema wadau hao wamepata muda mwafaka wa kujadili mwelekeo wa jinsi mradi utakavyotekelezwa na kujadiliana namna bora ya kutatua changamoto zitakazojitokeza katika halmashauri zao.

Mratibu wa Mradi wa LTIP, Bw. Joseph Shewiyo akizungumza na wadau wa ardhi (hawapo pichani) kujadili namna ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika Mkoa wa Tabora wakiongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Usawa Wa Kijinsia Katika Umiliki Wa Ardhi Kwa Ustawi Wa Jamii Yetu’’

Mkutano huu umekuja muda muafaka katika mkoa wetu hasa mwezi huu wa Machi ambao unaenda sanjari na Siku ya Wanawake Duniani yanayoongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Wekezakwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii’’ ni heshima kubwa mradi huu kutekelezwkatika wilaya zetu” amesema Balozi Dkt. Batilda.

 

 

Mradi huo unatekelezwa katika mkoa wa Tabora katika halmashauri za Kaliua, Sikonge, Uyui, Urambo, Nzega Mjini, Nzega Vijijini na Manispaa ya Tabora.

 

Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa mkoa huo upo mstari wa mbele katika kutekeleza mradi wa Uboreshaji wa Usalama wa Milki za Ardhi kwa maendeleo ya wananchi wa mkoa huo. 

 

Baadhi ya wadau wa ardhi wakiwa kaika mkutano wa kujadili namna ya kutekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika Mkoa wa Tabora wakiongozwa na kaulimbiu inayosema ‘‘Usawa Wa Kijinsia Katika Umiliki Wa Ardhi Kwa Ustawi Wa Jamii Yetu’’

Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka watalaam wa sektaya ardhi washirikiane na viongozi wa Serikaliza mitaa na vijiji kuwapawananchi elimu kuhusumasuala ya ardhi ili kutoa taarifa sahihi ambazo zitasaidia kurahisisha utekelezaji wa mradi huo.

 

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa LTIP, Bw. Joseph Shewiyo amesema mradi huo unalenga kupanga matumizi ya ardhi kwa maendeleo ya vijiji na miji, kuhamasisha umiliki wa ardhi kwa pamoja, kuzingatia haki za makundi maalum katika umiliki wa ardhi pamoja na usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi.

 

Bw. Shewiyo ameongeza kuwa hadi sasa mradi huo umeongeza idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi kutoka asilimia 25 hadi 38 hali inayosaidia kufikia azma ya Serikali ya kuwaletea wananchi usawa wa kijinsia katika umiliki wa ardhi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi