[caption id="attachment_5897" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate Ole Nasha akizungumza wakati wa siku ya Korosho iliyofanyika leo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam. Siku hiyo imewekwa maalum ili kuwahamasisha wananchi kula Korosho.[/caption]
Frank Mvungi
Wakulima wa Korosho nchini wamejipatia zaidi ya shilingi bilioni 800 kutokana na mauzo nje ya nchi katika msimu uliopita wa mauzo zao hilo.
Takwimu hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Tate ole Nasha wakati akifungua madhimisho ya siku ya Korosho iliyoadhimishwa kama sehemu ya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, Barabara ya Kilwa.
[caption id="attachment_5898" align="aligncenter" width="750"]“Serikali imekuja na utaratibu wa kuagiza mbolea kwa mkupuo na pia tutaanza kutoa mbolea kwa bei elekezi. Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tunawainua wakulima wa Korosho na sekta ya kilimo kwa ujumla”, Aaisisitiza Ole Nasha.
Aliongeza kuwa tani elfu 18 za mbolea aina ya salfa zitatolewa kwa wakulima bila malipo katika msimu ujao wa korosho hali itakayosaidia kuwaongezea ari wakulima wa korosho ambalo ndilo zao lililoingizia Taifa fedha nyingi zaidi za kigeni msimu uliopita.
Katika kuwawekea wakulima mazingira wezeshi Mhe. Ole Nasha alisema Serikali imeondoa tozo zaidi ya 140 zilizokuwa kero kwa wakulima hapa nchini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kukuza kilimo kwa maendeleo ya viwanda na uzalishaji wa ajira.
“Kukua kwa kilimo kutasaidia kuongeza ajira kwa vijana wetu wanaohitimu masomo katika vyuo mbalimbali ndio maana tunaweka mkazo katika kukuza zao hili ambalo lina faida si za kibiashara tu bali pia katika kujenga afya ikiwemo kupunguza lehemu mwilini, uzito na kujenga kinga ya mwili”, alisisitiza Ole Nasha.
[caption id="attachment_5902" align="aligncenter" width="750"]Kwa kuzingatia umuhimu huo alitoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kula korosho kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakuza soko la ndani.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Kilimo) Mhandisi Methew Mtigumwe amesema siku ya Korosho katika maonesho ya Sabasaba ni muhimu kwa kuwa inawakutanisha wadau wa sekta hiyo kwa pamoja.
[caption id="attachment_5908" align="aligncenter" width="750"]Pia aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki maadhimisho hayo hali inayoonyesha kuwa sasa kuna mageuzi makubwa katika sekta hiyo.
Bei ya Korosho katika msimu uliopita kwa Kilogramu moja iliuzwa shilingi 4000/- hali inayoonesha kuwa wananchi wakiunga mkono juhudi za Serikali kwa kuzalisha kwa wingi na kuongeza thamani ya korosho wanazozalisha basi zao hilo linaweza kutoa mchango mkubwa zaidi katika kujenga uchumi wa viwanda.