Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakazi wa Makomeni Kota Washukuru Fursa ya Kuishi Miaka Mitano Bila Kulipa Kodi
Mar 23, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu – MAELEZO

Wakazi 644 wa Magomeni Kota wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fursa ya kuishi miaka mitano bure katika nyumba za kisasa.

Hayo yamesemwa leo na Mwakilishi wa wakazi hao, Bw. George Abel katika hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo zilizopo eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.

“Lakini mama ameelekeza taasisi zinazosimamia eneo hilo, tutakaa miezi mitatu bure bila kulipia huduma jumuishi, lakini mama ameelekeza kuwa yale yaliyosemwa na Serikali baada ya kuondoka hapa kwamba tutakaa miaka mitano bure yako palepale,”ameeleza Abel.

Pamoja na hilo, amesema kwamba Rais Samia amewafuta machozi wakazi wa nyumba hizo ambao wengi wao ni wazee na wajane.

“Mama anazidi kuupiga mwingi, wakati wowote kuanzia sasa tunakabidhiwa funguo,” amearifu Abel.

Mradi wa Magomeni Kota ulioanza Oktoba Mosi, 2016 umegharimu takriban shilingi bilioni 52.2 ukihusisha ujenzi wa majengo matano yenye ghorofa nane na tisa ambapo nyumba zilizokwepo hapo awali zilikuwa za kawaida.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi