Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wakaguzi wa Bio-Teknolojia ya Kisasa Wapewa Mafunzo
Oct 26, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37456" align="aligncenter" width="750"] Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (Katikati ) akimsikiliza Dkt. Woldeyesus Sinebo Jinore Afisa Mwandamizi wa Program ya Kilimo na Matumizi salama ya Bioteknojia kutoka Shirika la NEPAD wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu kutoka Wizara na Taasisi za Serikali mafunzo haya yamefanyika katika Hotel ya Morena Jijini Dodoma. Kulia Bw. Thomas Chali Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.[/caption]

Katika jitihada za kuendelea kukuza uelewa wa wadau na jamii nzima kuhusu matumizi salama ya teknolojia ya uhandisi jeni /bio-teknolijia ya kisasa, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Shirika la NEPAD chini ya Umoja wa Afrika hii leo wamefanya mafunzo kwa wataalamu kutoka  Wizara na Taasisi za Serikali kuhusu Usimamizi wa Matumizi Salama ya Teknolojia ya kisasa katika ngazi ya Utafiti (Management on Confined Field Trial for GM Crops)

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika jijini Dodoma na yamefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine, na kufuatiwa na mafunzo kwa vitendo katika kituo cha Utafiti wa Kilimo Makutopora, Dodoma

[caption id="attachment_37457" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya washiriki kutoka Wizara na Taasisi za Serikali waliohudhuria mafunzo juu ya Usimamizi wa Matumizi Salama ya Teknolojia ya kisasa katika ngazi ya Utafiti (Management on Confined Field Trial for GM Crops). Mafunzo hayo ya siku mbili yatafuatiwa na mafunzo kwa vitendo katika shamba la majaribio katika kituo cha Utafiti cha Makutupora.[/caption] [caption id="attachment_37458" align="aligncenter" width="750"] Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (mwenye tai nyekundu) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo kutoka Wizara na Taasisi za Serikali waliohudhuria mafunzo juu ya Usimamizi wa Matumizi Salama ya Teknolojia ya kisasa katika ngazi ya Utafiti[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi