Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wahariri wa Habari Waaswa Kuzingatia Matumizi ya Takwimu Rasmi
Sep 24, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_47272" align="aligncenter" width="1000"] Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 leo jijini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini wameaswa kuendelea kuzingatia matumizi ya takwimu rasmi katika kuelimisha umma  kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Akizungumza  wakati akifungua warsha kwa wahariri hao leo Jijini Dodoma, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt Albina Chuwa amesema kuwa dhamira ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni kuendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika matumizi ya takwimu zinazozalishwa hapa nchini.

[caption id="attachment_47273" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Fedha na Utawala na Masoko toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw.Daniel Andrew akielezea madhumuni ya warsha ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 wakati wa hafla ufunguzi wa warsha hiyo leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47274" align="aligncenter" width="1000"] Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Emilian Karugendo akielezea madhumuni ya warsha ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 wakati wa hafla ufunguzi wa warsha hiyo leo jijini Dodoma.[/caption]

“NBS iko tayari kusaidia asasi za kiraia ili kuzalisha takwimu sahihi kwa kutumia miongozo na kanuni za ukusanyaji na uchakataji wa takwimu hizo kwa maslahi ya wananchi ” Alisisitiza Dkt Chuwa

Akifafanua Dkt. Chuwa amesema kuwa takwimu ni suala la kisayansi hivyo linahitaji utaalamu katika kukusanya, kuzichakata na kuzitoa kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa Ofisi hiyo itaendelea kuvijengea uwezo Vyombo vya Habari ili viweze kuelimisha umma kwa kutoa taarifa sahihi na kutumia takwimu rasmi.

[caption id="attachment_47275" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Said Ameir akitoa ufafanuzi kuhusu malengo ya warsha ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2018 na 2019 wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo leo tarehe 24 Septemba 2019 jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47276" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia hotuba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47277" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya Wahariri na wawakilishi wa vyombo vya habari wakifuatilia hotuba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47278" align="aligncenter" width="1000"] Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari kutoka Dodoma mara baada ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa Wahariri hao kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_47279" align="aligncenter" width="1000"] Mtakwimu Mkuu wa Serikali toka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) mara baada ya ufunguzi wa warsha ya siku mbili kwa Wahariri hao kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 jijini Dodoma. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO).[/caption]

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala, Fedha na Masoko wa NBS, Bw. Daniel Andrew amesema kuwa Ofisi yao inatambua umuhimu wa Vyombo vya Habari katika kuelimisha umma kuhusu masuala ya takwimu na kuchochea maendeleo.

Aliongeza kuwa warsha kwa wahariri hao inalenga pamoja na mambo mengine kuwajengea uwezo kuhusu mabadiliko ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 yaliyofanyika mwaka 2018 na 2019 na faida zake katika kuchochea ukuaji wa uchumi.

Aidha, Mabadiliko hayo yamechangia baadhi ya nchi kuja kujifunza faida zinazotokana na mabadiliko hayo kwa maslahi ya wananchi.

Warsha hiyo imewashirikisha Wahariri wa Vyombo vya Habari kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wakiwemo kutoka katika Televisheni, Radio, Magazeti na mitandao ya Kijamii.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi