Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wafugaji Watakiwa Kutembea Kifua Mbele 
Nov 03, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21626" align="aligncenter" width="750"] Picha ya pamoja ikimuonyesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina, Mkuu wa Wialaya ya Biharamulo Bi Saada Malunde baada ya zoezi la kukagua uvamizi wa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamuro, wengine katika picha ni askari wanyamapori wa pori hilo.[/caption]

Mwandishi Maalum - KATERERO

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhanga Mpina amewataka wafugaji nchini kutembea kifua mbele kwa kumpata yeye kama Waziri mwenye dhamana ya Mifugo, Mpina ameyasema hayo leo aliposhiriki katika zoezi la kupiga chapa Mifugo  katika Kijiji cha Kyelwa kilichopo katika kata ya Katerero Halmashauri ya Wilaya Bukoba mkoani Kagera,  na kuwataka viongozi kuzingatia maadili wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuepuka hujuma na ubaguzi kwa wafugaji.

Waziri Mpina alishiriki katika  zoezi la uwekaji alama katika mifugo na kuwataka wafugaji wengi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo kwani  lina faida kwa wafugaji kwakuwa litaweza kuwasiadia kuepuka maambukizi ya magonjwa ya wanyama kwa mifugo yao kutokana na kuchanganyikana na mifugo mingine sambamba na kuepuka upotevu wa mifugo.

Akiongea katika zoezi hilo Diwani wa Kata ya Katerero Bw. Nuru Abdul Kabendera alisema kuwa, amefurahishwa na ziara ya Waziri Mpina katika kata ya Katerero kwani ni mara ya kwanza kwa kata hiyo kupata ugeni kutoka katika ngazi ya juu ya serikali na kumuomba Mpina kupitia Wizara yake kutatua changamoto inayoikabili kata hiyo la josho la kuoshea ng’ombe ambapo Waziri Mpina amehaidi kuitatua.

[caption id="attachment_21627" align="aligncenter" width="750"] Mpina akiongea na wanahabari mara baada ya ukaguzi wa oparesheni ondoa mifugo katika sehemu ya pori la Bugiri Biharamulo, Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Saada Malunde.[/caption] [caption id="attachment_21628" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya ng'ombe aliyepigwa chapa katika kata ya katerero kijijini Kyelwa leo.[/caption] [caption id="attachment_21629" align="aligncenter" width="750"] Waziri Mpina na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Bukoba wakielekea katika zoezi la upigaji chapa ng'ombe katika kata ya katerero kijijini Kyelwa leo.[/caption]

Katika hatua nyingine Waziri Mpina ametembelea mapori ya Burigi yaliyopo wilayani Biharamulo ambapo ameupongeza uongozi wa mkoa kwa operesheni iliyofanyika ya kuondoa mifugo katika mapori tengefu na hifadhi za misitu ambapo amewashuhudia wanyama pori ambao tayari wamerejea katika mapori hayo huku Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Saada Malunde Akiwataka wananchi wa Wilaya hiyo kutoa ushirikiano katika zoezi la kuondoa mifugo.

Aidha, Waziri Mpina amewataka wakuu wa Mikoa ya mipakani kuwasilisha kwake taarifa ya uondoshwaji wa mifugo katika mikoa yao mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la operesheni ondoa mifugo.

Waziri amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera na kuagiza kuwa  mifugo yote iliyokamatwa kutoka nje ya nchi itaifishwe na kupigwa mnada haraka sana kwa mujibu wa sheria.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi