Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wafanyakazi JKCI Watakiwa Kujiendeleza Kielimu Kuendana na Sayansi na Teknolojia
Dec 20, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39137" align="aligncenter" width="750"] Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji Dkt. Bashir Nyangasa (hayupo pichani) akieleza jinsi upasuaji wa moyo unavyofanyika kwa wagonjwa wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.[/caption]

Na Mwandishi Maalum – Dar es Salaam

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wametakiwa kujiendeleza kielimu ili waweze kutoa huduma bora zaidi na za kisasa  kwa wagonjwa zinazoendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Rai hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza katika kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Prof. Janabi alisema utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa na wananchi unaendana na mabadiliko  ya sayansi na teknolojia hivyo basi ni jukumu la wafanyakazi hao kuhakikisha wanajiendeleza kielimu   kwa njia ya mtandao, elimu ya masafa marefu au kwenda darasani kusoma.

[caption id="attachment_39138" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delila Kimambo akieleza jinsi huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo inavyotolewa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.[/caption]

“Ukiwa na elimu ya kutosha ambayo itaendana na Dunia ya sasa utaweza kufanya kazi zako kiufanisi, kutoa huduma bora kwa wagonjwa na wananchi na kuongeza mapatao . Nawasisitiza wafanyakazi wenzangu tumieni muda wenu wa ziada mnaoupata kujiendeleza kielimu”, alisisitiza Prof. Janabi.

Prof. Janabi pia aliwahimiza wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii, kuwahi kazini na kutumia muda wao wa kazi  kutoa huduma kwa wananchi na siyo vinginevyo huku wakifuata sheria na taratibu za utumishi wa Umma na maadili ya kazi zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi Robert Mallya alisema kurugenzi yake itaendelea kutoa mafunzo kwa maafisa uuguzi ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa moyo ili wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo  waendelee kupewa  huduma bora zaidi ya kiwango cha kimataifa.

[caption id="attachment_39139" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akieleza jinsi maafisa uuguzi wanavyohudumia wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_39140" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo.[/caption]

“Kama mnavyofahamu wauguzi ndiyo wanaokaa muda mwingi na wagonjwa walioko wodini ili wagonjwa wetu waweze kupata huduma bora za  kiwango cha kimataifa tutaendelea  kutoa  mafunzo ya mara kwa mara ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa moyo”, alisema Mallya.

Naye Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tiba Shirikishi Dkt. Delila Kimambo alisema Kurugenzi yake kwa mwaka 2018  imefanikiwa kufungua maabara kubwa yenye mashine za kisasa ambazo kupitia wataalamu waliopo watapima  magonjwa mbalimbali kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

“Kupatikana  kwa mashine  za kisasa za maabara kutasaidia wagonjwa wetu kupimwa magonjwa yote katika Taasisi yetu tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyumba ambapo wagonjwa iliwalazimu kupima vipimo vingine katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili”, alisema Dkt. Delila.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi