Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wafanyabiashara Jijini Arusha Waunga Mkono Operesheni ya Ukusanyaji Mapato
Sep 23, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_35566" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr Maulid Suleiman Madeni akiongea na viongozi wa wafanyabiashara wa Jiji la Arusha katika Mkutano uliofanyika hapo Juzi Tarehe 21/09/2018, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro[/caption] [caption id="attachment_35567" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya viongozi wa wafanyabiashara wa Jiji la Arusha wakifuatilia kwa makini maagizo waliyokuwa wakipatiwa wakati wa mkutano huo uliofanyika juzi katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya.[/caption]

Na. Fatuma  IbrahimuArusha.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Grabriel F. Daqarro pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni juzi Tarehe 21/09/2018 waliitisha mkutano na wafanyabiashara wa Jiji la Arusha kujadili hatma ya wadaiwa sugu wa mapato ya serikali na kuwataka kufanikisha zoezi la ulipaji ushuru wa maduka na pia kuzingatia kipengele No. 15 kwenye mkataba kinachoanisha kuwa mkataba unaweza kuvunjika pale ushuru wa duka unapocheleweshwa kulipwa kwa muda sahihi.

Mhe. Daqaro ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mkutano huo ametilia msisitizo operation ya ukusanyaji mapato iliyoanzishwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni na kuwataka wafanya biashara kulipa madeni yote ya nyuma wanaodaiwa .

“Nawapa muda wa siku 21 kulipa madeni yote kama sheria inavyosema au tutafuata agizo la kuvunja mkataba kama ilivyoainishwa kwenye kipengele No. 15 kwenye mkataba wenu na Halmashauri” alisema Mhe. Daqaro.

[caption id="attachment_35568" align="aligncenter" width="750"] Mfanyabiashara Dominic Mollel (kulia) akishikana mkono na Mkurugenzi wa Jiji Dr. Maulid Suleiman Madeni (kushoto) kama ishara ya kumaliza tofauti zao zilizoweza kujitokeza baada ya mfanyabiashara huyo kukwamisha operesheni ya ukusanyajia mapato.[/caption]

Sambamba na hilo Mhe. Daqaro ameagiza kufuatiliwa kwa vibanda ambavyo havina leseni au mikataba ambavyo viko maeneo ya Kwa Morombo Jijini Arusha ili wafanyabiashara wa vibanda hivyo walipe ushuru na madeni wanayodaiwa na kufanikisha maendeleo ya Jiji na nchi nzima kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni aliwaambia wafanyabiashara kuwa operesheni ya ukusanyaji wa mapato aliyoianzisha haina lengo la kuwakandamiza wafanyabiashara bali kuhakikisha mapato yanaongezeka ili kumsaidia mheshimiwa Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutekeleza majukumu yake ya kuboresha miundombinu ya kiuchumi kwa faida ya wananchi wote sekta nyeti za Elimu na Huduma za afya na si vinginevyo.

[caption id="attachment_35569" align="aligncenter" width="750"] Ndg. Dominic Mollel akiwa analipa deni lake analodaiwa la ushuru wa kibanda ndani ya kikao kuonyesha utii na kuunga mkono operesheni hiyo ya ukusanyaji wa mapato iliyoanzishwa na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni.[/caption]

“Hatuna ugomvi na mfanyabiashara yoyote yule isipokuwa sitavumilia kuona mtu ama kikundi cha watu fulani aidha wanakataa au kuchelewesha ulipaji ushuru au kodi ya Serikali au kutaka kuzuia operesheni zenye manufaa za aina hii za ukusanyaji wa mapato” alisema Dr Madeni. Naye mfanyabiashara Domonic Mollel aliyeingia katika migogoro na Mkurugenzi siku za nyuma kwa kosa la kumkwamisha Mkurugenzi kutekeleza operesheni yake ya ukusanyaji wa mapato na kutishia usalama wa Mkurugenzi huyo aliahidi kushirikiana bega kwa bega na Serikali hii pamoja na viongozi wa Jiji la Arusha kulipa deni lake na kuhakasisha wafanyabiashara wote wa Jiji wanalipa kodi bila kuchelewa.

Opereshen ya ukusanyaji wa mapato ilianzishwa rasmi na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dr. Maulid Suleiman Madeni Tarehe 10/9/2018, Operesheni hii ni endelevu na inalenga kubaini wadaiwa sugu pamoja na kusimamia mapato ya Halmashauri ili yasaidie kuendeleza mafanikio ya miradi mbalimbali ya Jiji la Arusha.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi