Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wafamasia nchini Waaswa kutekeleza majukumu yao kwa Weledi
Sep 25, 2018
Na Msemaji Mkuu

Frank  Mvungi- MAELEZO, Dodoma

Wafamasia nchini waaswa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano  kutoa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge  itimie kwa wakati.

Akizungumza katika mahojiano maalum leo Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya wafamasia Duniani, Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania Bi Elizabeth Shekalaghe amesema kuwa maadhimisho ya siku  ya wafamasia yanalenga kufanya tathmini ya utendaji wao ili kuona namna bora ya kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Msajili wa Baraza  Famasi Tanzania Bi Elizabeth  Shekalaghe (kushoto) akisisitiza jambo kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bw. Juma Mnwele leo Jijini Dodoma wakati alipotembelea Banda la Baraza hilo lililopo katika Viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

“Siku hii ni muhimu kwa Wafamasia wote kwani inatuleta pamoja si tu kusherehekea bali kuangalia na kufanya tathmini ya kina kuhusu utendaji wetu wa kila siku katika kuwahudumia wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na hatimaye tuendelee kuboresha utendaji wetu” .Alisisitiza Bi Shekalaghe

Akifafanua amesema kuwa, jukumu la kutoa huduma bora kwa wananchi ni nyenzo muhimu katika kuchochea ukuaji wa kada hiyo na  ustawi wa jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Kahama Bw. Anderson Msumba akisisitiza jambo kwa Msajili wa Baraza  Famasi Tanzania Bi Elizabeth  Shekalaghe leo Jijini Dodoma ikiwa ni siku ya wafamasia Duniani ambapo Baraza hilo linashiriki kutoa elimu kwa wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT)  leo Jijini Dodoma.

Pia alitoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kupata huduma katika maduka yaliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zinazosimamia kada hiyo.

Baraza la Famasi ni taasisi ya kitaaluma chini ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, lililoundwa chini ya kifungu Na. 2 cha Sheria ya Famasi Cap 311 baada ya Sheria ya Famasi ya mwaka 2002 kufutwa. Baraza limepewa jukumu la kusimamia taaluma ya famasi ikiwemo usajili wa maduka ya dawa kazi ambayo imeanza kutekelezwa rasmi mwaka 2012. Katika kutekeleza Sheria ya Famasi, Baraza linashirikiana na watendaji wa Halmashauri na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

[caption id="attachment_35673" align="aligncenter" width="834"] Msajili wa Baraza  Famasi Tanzania Bi Elizabeth  Shekalaghe akiwa kwenye picha ya pamoja na wafamasia wa Baraza hilo wanaoshiriki kutoa elimu kuhusu majukumu ya Baraza hilo  katika mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT)  leo Jijini Dodoma.[/caption]  

Sehemu ya majukumu ya Baraza hili  ni Kusajili wanataaluma wote (Wafamasia) , Kusajili majengo ya kutolea huduma za dawa,  Kuweka na kusimamia viwango vya utendaji wa taaluma ya famasi , Kupitia mitaala na kuweka viwango vya elimu kwa wanataaluma wa famasi na kuhakikisha vina ubora unaohitajika, Kuhamasisha na kusimamia maadili ya taaluma ya famasi .

  [caption id="attachment_35675" align="aligncenter" width="900"] Mfamasia wa Baraza la Famasi Tanzania Bi Suma Jairo akisisitiza jambo kwa mmoja wananchi waliotembelea Banda la Baraza hilo lililopo katika Viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.[/caption]

Majukumu mengine ni Kujibu na kushughulikia masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi , Kulinda na kuhamasisha huduma za taaluma ya famasi zitolewe kulingana na viwango na maadili, Kuweka na kutunza taarifa za wanataaluma wote waliosajiliwa, Kuimarisha uhusiano na ushirikiano na taasisi

Msajili wa Baraza  Famasi Tanzania Bi Elizabeth  Shekalaghe akisisitiz jambo kwa Maofisa wa Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA) leo Jijini Dodoma ikiwa ni siku ya wafamasia Duniani , Baraza hilo linashiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT)  unaoendelea  Jijini Dodoma.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi