Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadau Watakiwa Kuzingatia Matumizi ya Kemikali Bashirifu
Aug 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46306" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias (kulia) akifungua Mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti na Sekta Binafsi katika kuzuia uchepushaji wa kemikali bashirifu uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mkutano wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam.[/caption]

Na: Mwandishi Wetu

Wadau wanaoagiza, kusafirisha na kutumia kemikali bashirifu nchini wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya kemikali hizo ili kuepusha kuchepushwa na kutumika kinyume na matumizi yaliyolengwa ikiwemo kutengeneza dawa za kulevya.

Akiongea kwa niaba ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti na wadau wa Sekta binafsi katika kuzuia uchepushaji wa kemikali bashirifu, Kaimu Mkurugenzi wa Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, David Elias, alisema Serikali imekuwa ikitumia njia mbalimbali ili kuongeza jitihada ikiwemo kutunga Sheria kwa lengo la kupambana na kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu ambazo zinaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.

  [caption id="attachment_46309" align="aligncenter" width="750"] Meneja wa Ukaguzi wa Kemikali, Fidelis Segumba (kulia) akiwasilisha mada kuhusu Sheria zinazohusiana na Udhibiti wa Kemikali Bashirifu.[/caption] [caption id="attachment_46310" align="aligncenter" width="750"] Mwezeshaji kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba, Marcia Awe (kulia) akiwasilisha mada wakati wa mkutano huo.[/caption]

“Kama njia mojawapo ya kusimamia mwenendo wa biashara na matumizi ya kemikali bashirifu, Serikali kupitia Mamlaka za udhibiti imeunda Sheria na Kanuni mbalimbali za kusimamia na kudhibiti uingizaji, usambazaji, usafirishaji, utumiaji, utekelezaji na usafirishaji wa kemikali nje ya nchi. Hivyo, ni muhimu kwa wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na kemikalimmbalimbali ikiwa pamoja na kemikali bashirifu, kuelewa Sheria na kanuni ili kuzitekeleza.”

Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias, alisema mkutano huo utatoa ufafanuzi juu ya uchepushaji wa kemikali bashirifu na ushirikishwaji wa sekta binafsi katika udhibiti.

“Ni matumaini yetu kwamba wadau mliopo kwenye mkutano huu mtapata uelewa wa kemikali bashirifu ni nini na umuhimu wa kudhibiti, uelewa wa Sheria na kanuni za udhibiti na mbinu zinazotumika katika kuchepusha kemikali hizo, hivyo naomba muwe huru kujadiliana, kutoa mapendekezo ya namna bora ya kushirikiana kati ya Mamlaka za Udhibiti na Sekta binafsi ili kufukia lengo la Serikali katika kudhibiti mianya yote inayoruhusu uchepushwaji wa kemikali bashirifu” alimaliza.

  [caption id="attachment_46312" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa mkutano wakiuliza maswali na ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyowasilishwa wakati wa mkutano huo.[/caption] [caption id="attachment_46313" align="aligncenter" width="750"] Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai, Bertha Mamuya (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa hoja na maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wadau walioshiriki katika mkutano huo.[/caption] [caption id="attachment_46314" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya wadau walioshiriki mkutano wakifuatilia mada wakati wa mkutano.[/caption] [caption id="attachment_46308" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias (aliyekaa kulia) na Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai, Bertha Mamuya (aliyekaa kushoto) wakiwa pamoja na washiriki wa mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka za Udhibiti na Sekta Binafsi katika kuzuia uchepushaji wa kemikali bashirifu uliofanyika leo, Dar es Salaam.[/caption]

Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai kutoka Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Bertha Mamuya, akiongea kwa niaba ya Kamishna Jenerali, alisema wanaamini ushirikishwaji wa wadau wa kemikali utaongeza ufanisi katika kudhibiti uchepushaji wa kemikali.

“Kama Serikali tunaamini ushirikiano na wadau wa kemikali katika kujisimamia na kushirikiana na Mamlaka husika kutaongeza ufanisi katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali bashirifu hivyo kufanikisha vita dhidi ya dawa za kulevya. Ni matumaini yangu majadiliano katika mkutano huu yatachagiza nia njema ya uanzishwaji wa ushirikiano wa hiari kati ya wadau na Mamlaka za udhibiti ili kufanikisha lengo la Serikali katika upatikanaji wa dawa za kulevya.”

Mamlaka za udhibiti zilizoshiriki katika mkutano huo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Baraza la Famasia Tanzania, Bohari ya Dawa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba na kuhusisha wadau mia moja wanaojihusisha na shughuli kemikali na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi