Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadau Wakabidhi Chumba Maalum cha Upasuaji cha Watoto
Aug 27, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_46280" align="aligncenter" width="750"] 1. Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Umma na binafsi wa Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Wonanji Vivian akitoa hotuba wakati wa hafla ya kupokea chumba maalum cha upasuaji kwa watoto wemye vichwa vikubwa na Mgongo wazi MOI[/caption] [caption id="attachment_46281" align="aligncenter" width="750"] 2. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface akitoa hotuba wakati wa hafla ya kupokea chumba maalum cha upasuaji kwa watoto wemye vichwa vikubwa na Mgongo wazi MOI[/caption]

Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Umma na binafsi wa Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Wonanji Vivian leo amepokea chumba maalum cha upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ambacho kimekarabatiwa na MOI pamoja na wadau kwa zaidi ya Tshs Milioni 500.

Dkt. Wonanji amewashukuru wadau ,wafadhili pamoja na washirika wa MOI ambao wameshiriki katika ukarabatati na uanzishaji wa chumba hicho maalum.

“Leo tumekusanyika hapa kwa lengo moja kuu la kupokea rasmi chumba cha upasuaji kwaajili ya Watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, hii ni hatua kubwa hapa nchini, nafahamu chumba hicho kilishaanza kutumika lakini leo kinakabidhiwa rasmi hongereni na ahsanteni wote mlioshiriki katika hili.” Alisema Dkt Wonanji.

[caption id="attachment_46282" align="aligncenter" width="750"] 3. Dkt Wonanji Vivian akikata utepe kuashiria kupokea chumba maalum cha uapsuaji cha watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi katika MOI[/caption] [caption id="attachment_46283" align="aligncenter" width="750"] 4. Wajumbe wa kamati ya uendeshaji ya MOI (Management comitee) ya MOI pamoja na wadau wengine wakifuatilia hotuba katika hafla ya kupokea chumba maalum cha upasuaji cha watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi MOI[/caption]

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema chumba hicho kimejengwa kwa ushirikiano na wadau mbalimbali ambao ni chama cha Wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Tanzania ASBATH, Ndugu AKheri Kakoo kutoka Shia khoja athna asheri Muslim community, Cure International na Ubalozi wa Kuwait hapa nchini.

“Chumba hiki kilianza kutumika mwezi Aprili na tayari watoto zaidi ya 352 wamefanyiwa upasuaji, ni matumaini yetu kwamba tutawahudumia watoto wengi zaidi ,awali tuliwafanyia upasuaji watoto 45-50 kwa mwezi sasa hivi tunawafanyia upsauji watoto 85-100 kwa mwezi hii imeondoa changamoto ya kusubiri upasuaji kwa muda mrefu.” Alisema Dkt. Boniface.

[caption id="attachment_46284" align="aligncenter" width="750"] 5. Dkt Wonanji Vivian akiwa katikati pamja na Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface wakiwa picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya uendeshaji ya MOI pamoja na Wadau mbalimbali wa MOI.[/caption]

Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi Tanzania Bw. Hakeem Bayakub amesema Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba zaidi ya watoto 4800 wanazaliwa na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi kila mwaka hapa nchini, ambapo idadi ya watoto wanakwenda hospitali kupata huduma imeongezeka maradufu kutokana na uelewa kuongezeka.

Imetolewa.

Kitengo cha Uhusiano MOI

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi