Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wadau Wahamasishwa Matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi Kutoa Huduma kwa Jamii
Jun 03, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu - WHMTH

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojhia ya Habari imekutana na wadau wa Mfumo wa Anwani za Makazi katikati ya wiki hii jijini Dodoma kwa lengo la kuwapitisha hatua za utekelezaji wa mfumo huo na kuhamasisha matumizi ya mfumo huo katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi

Akizungumza katika kikao kazi hicho Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO wa Wizara hiyo, Bwana Gerson Msigwa ametoa rai kwa wadau hao kushirikiana na Wizara kuutangaza na kuhamasisha watanzania kutumia miundombinu ya Mfumo wa Anwani za Makazi pamoja na mfumo wa kidijitali wa NaPA kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii

“Niwahakikishie kuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari muda wote tutakuwa tayari kusikiliza na kupokea maoni ya wadau wetu wote wanaoutumia mfumo wa Anwani za Makazi kutoa, kutafuta au kupokea huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi, hivyo tushirikiane kuutangaza na kuhamasisha watanzania kutumia mfumo huu”, amezungumza Msigwa.

Amesema kuwa Mfumo huo ni moja ya miradi mikubwa inayotekelezwa na Wizara hiyo na baadae kutolewa maelekezo ya kutekelezwa kwa njia ya operesheni, ili usaidie kuboresha takwimu za Sensa ya Watu na Makazi inayofanyika mwezi Agosti mwaka huu wa 2022

Msigwa ameipongeza timu nzima ya Wizara pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri ya uratibu na kutengeneza mfumo wa kidijitali wa utambuzi wa NaPA ambao utasaidia kuboresha utoaji wa huduma na kuifungua nchi katika uchumi usio na mipaka uchumi wa kidijitali

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Mhandisi Clarence Ichwekeleza amesema kuwa takwimu zinaonesha utekelezaji wa operesheni ya Anwani za Makazi umefikia asilimia 106. 9 na Wizara inaendelea na zoezi la kuhakikina kuswafisha taarifa zilizokusanywa za Anwani za makazi ambapo mpaka sasa jumla ya Anwani 12,381,383 zimeshakusanywa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi