Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wabunge Tabora Wamshukuru Rais kwa Kuwajengea Miundombinu
May 19, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Adelina Johnbosco

Wabunge mkoani Tabora wametoka shukrani zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani humo, huku wakionesha furaha yao zaidi kwenye miundombinu ya barabara. 

Mbunge wa Sikonge, Mhe. George Kakunda amesema Rais ameiheshimisha Tabora na kuifananisha na hadhi yake ya kuwa Makao Makuu ya Kanda ya Magharibi.

"Tunatoa shukrani zetu kwa Serikali yako Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha ujenzi wa barabara tatu kuu, barabara ya kutoka Tabora kupitia Dodoma kwenda Dar es Salaam, barabara ya kutoka Tabora kwenda Shinyanga hadi Mwanza kupitia Nzega, na barabara ya kutoka Tabora kwenda Mpanda kupitia Sikonge na barabara zingine zinaendelea kujengwa ikiwemo ujenzi wa reli ya SGR, asante sana", amesisitiza Mhe. Kakunda.

Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Hawa Mwaifunga amempongeza na kumshukuru Rais Samia kwa kuwasaidia Watanzania wa hali zote.

"Haya ni maendeleo ya watu, umepambana kuendeleza miradi yote mliyoianza tangu Awamu ya Tano na unaendelea kuhakikisha unatekeleza miradi mipya, hii inamgusa kila Mtanzania bila ubaguzi wowote", alisema Mhe. Mwaifunga

Haya yanajiri ikiwa ni hitimisho la siku tatu za ziara ya kikazi ya Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani Tabora ambapo amezindua miundombinu ya barabara na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo mkoani humo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi