[caption id="attachment_26610" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia majibu ya mama mjamzito kuhusu upatikanaji bure wa vifaa vya kujifungulia, kushoto ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Kasulu Dkt Dastan.Ndugulile akisalimiana na mmoja kati ya wagonjwa katika Hospitali ya Kasulu Mkoani Kigoma.[/caption]
Na.Mwandishi Wetu. KIGOMA
Serikali imeviagiza vyombo vya usalama na kamati za Afya za vijiji kuimarisha mifumo yote ya udhibiti wa upotevu wa dawa nchini, kwa kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba ili kuondoa ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ziara yake katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma ya kukagua utoaji huduma za afya na kufuatilia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya jamii ambao inasisitiza ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi.
“Niwaombe sana ndugu zangu wananchi tuwe walinzi, hiyo dawa ingeweza kukusaidia wewe, au ndugu yako, hivyo kushiriki katika ubadhilifu huo ni kujiumiza mwenyewe” alisema Dkt. Ndugulile.
[caption id="attachment_26612" align="aligncenter" width="750"]Katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto Dkt. Faustine amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewekeza kiasi cha shilingi milioni 400 katika Halmashauri 175, kikiwemo kituo cha Afya cha Uvinza , fedha zitakazotumika kuboresha na kujenga vyumba vya kutolea huduma ya dharura wakati wa kujifungua, nyumba za watumishi pamoja na maabara.
Dkt. Faustine aliendelea kusema kwamba, Serikali inaendelea kufanya vizuri barani Afrika na Dunia kwa ujumla kwa upande wa utoaji chanjo, kwani imefikia asilimia 97 ya walengwa wote wanaohitaji chanjo nchini jambo linalosaidia kutunza Afya za watu katika jamii.
Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa anatambua uhaba wa watumishi unaovikabili vituo vingi vya Afya katika Wilaya ya Uvinza ambao umefikia asilimia 66 na kuahidi kulifanyia kazi ombi hilo ili kupunguza changamoto katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
[caption id="attachment_26614" align="aligncenter" width="750"]