Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Vyombo vya Habari Vyaaswa Kuwa na Watumishi Wakutosha Mkoani Dodoma
Jan 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_27374" align="aligncenter" width="956"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya Habari Mkoani Dodoma mapema leo.kulia ni Mkuu wa TBC Kanda ya Kati Bw. Bakari Msulwa.[/caption]

Na: Beatrice Lyimo

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbas ametoa wito kwa vyombo vyote vya habari mkoani Dodoma na kwingine nchini kuhakikisha wanakuwa na wafanyakazi wa kutosha watakaokidhi mahitaji kutokana na Serikali kuhamia Dodoma.

Dkt. Abbas ametoa wito huo leo mjini Dodoma wakati wa muendelezo wa ziara yake kutembelea vyombo vya habari mkoani humo ambapo leo ametembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Uhuru Redio pamoja na Uhuru gazeti.

“Lengo la ziara yangu ni kuona na kujua changamoto za kiutendaji mnazao kutana nazo pamoja na jinsi gani mmejipanga juu ya ujio wa Serikali kuhamia Dodoma kwani matukio mengi ya kiserikali yatafanyika Mkoani hapa” ameongeza Dkt. Abbasi.

[caption id="attachment_27375" align="aligncenter" width="750"] . Mmoja wa Mafundi Mitambo wa TBC Kanda ya Kati Bw. Mbijimi Mzungu akitoa maelezo kwa. Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kuhusu namna mitambo ya Shirika hilo inavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Shirika hilo mapema leo.[/caption] [caption id="attachment_27376" align="aligncenter" width="910"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akikagua vifaa vilivyopo ndani ya moja ya Studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma wakati wa ziara yake mapema leo[/caption]

Aidha, Dkt. Abbas amevitaka vyombo vya Habari kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano, ubunifu na kufuata maadili katika utendaji kazi hasa katika wakati huu wa mageuzi makubwa nchini.

“Katika mabadiliko au mageuzi yeyote hasa yanayoendelea sasa nchini kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake mahali pake pa kazi ili katika Tanzania ijayo ajivunie si kwa kuwa mlalamishi tu bali ajivunie kuwa naye alishiriki ipasavyo katika safari hii ya mabadiliko” amesisitiza Dkt. Abbas.

Dkt. Abbas ameongeza kuwa “Kwa upande wa habari mimi nimepewa jukumu la kusimamia maadili katika vyombo vya habari hivyo nasimamia na kufuata sheria na busara katika kila jambo linalohusu sekta ya habari ndio maana hatuchukui hatua tu bali tunashauriana na kuonyana kwanza pale wachache wanapokengeuka”.

[caption id="attachment_27377" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Kanda ya Kati Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_27378" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na watumishi wa redio na gazeti la Uhuru Mkoani Dodoma mapema leo wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya Habari.Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya Pamoja na Watumishi wa gazeti la Uhuru Mkoani Dodoma mara baada yakuwatembelea mapema leo. (Picha zote na Frank Mvungi)[/caption]

Mbali na hayo Dkt. Abbas amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anapambana na azma ya kupigania nchi  kujitegemea na si kutegemea nchi za nje kwa maisha yetu yote hivyo vyombo vya habari vinajukumu la kupongeza pale Serikali inapotimiza kazi vyema na kukosoa  pale ambapo Serikali inakosea lakini si kwa kukejeli, kutusi au chombo cha habari kuonekana kinafanya inda.

Ziara hiyo itaendelea kesho mkoani humo ambapo Dkt. Abbas atatembelea vituo vya Redio Alternative Fm (AFm) na Redio Nyemo Fm.

   

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi