[caption id="attachment_6200" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. George Simbachawene akifafanua jambo wakati akizungumza za viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kondoa kwenye kikao maalumu alichokiitisha kutazama chanzo cha migogoro Wilayani humo. (Picha na: OR -TAMISEMI)[/caption]
Na. Mwandishi Wetu
Viongozi katika halmashauri nchini wametakiwa kuacha migogoro isiyokuwa na tija na badala yake waungane ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene alipokuwa akiongea na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kondoa akiwemo Mkuu wa Wilaya, Madiwani, Mbunge, viongozi wa dini pamoja na wazee wa mji huo kwa lengo kuwasikiliza viongozi hao ili kujua nini chanzo cha migogoro ya mara kwa mara katika halmashauri ya Mji wa Kondoa.
“Wilaya yenu imekuwa ni miongoni mwa wilaya kadhaa nchini ambazo zimekuwa na tatizo la kiuongozi kitu ambacho kisababisha kusua sua kwa maendeleo katika halmashauri yenu. Kupitia kikao hiki ningependa kufahamu kutoka kwenu nini hasa sababu ya migogoro hii na kama ikiwezekana tupate suluhisho la migogoro hii ili tuendelee kufanya kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi,”alisema Waziri.
[caption id="attachment_6202" align="aligncenter" width="750"]Miongoni mwa migogoro iliyopo ni baada ya madiwani wa halmashauri ya mji huo kumuondoa ktika uongozi Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Bw. Alhaji Omar Kariati ambapo baada ya kuondolewa kwa Mwenyeki huyo madiwani wamegawanyika katika makundi mawili ya wanaaounga mkono kuondolewa kwake na wale kitu kinachopunguza ufanisi katika utendaji kazi katika halmashauri hiyo.
Akichangia mada katika kikao hicho, Sheikh Twalha, sheikh mkuu wa mkoa msaafu alimshukuru Mhe. Waziri kwa kuitisha kikao hicho na kuwataka viongozi kuitisha vikao vya namna hiyo mara kwa mara ili kutatua migogoro kabla haijawa mikubwa na kuzuia maendeleo.
[caption id="attachment_6205" align="aligncenter" width="750"]Vile vile aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kuungana na kufanya kazi kwa pamoja kwani uongozi ni dhamana hivyo kuna kila sababu ya kufanya kazi kwa pamoja.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bi. Sezaria Veneranda Makota, amewataka viongozi wa halmashauri hiyo kusameheana kwa yale yote yaliyopita na badala yake warudi kuwa kitu kimoja na kuwatumikia wananchi kwani kila mmoja yupo katika nafasi yake ili kuwatumikia wananchi.
Akifunga kikao hicho kilichodumu kwa zaidi ya saa nane Mheshimiwa Simbachawene aliwaagiza viongozi wote wa halmashauri hiyo kutambua mipaka ya kiuongozi baina yao kwani kila mmoja ana madaraka, majukumu na vilevile kila mmoja ana nafasi yake na anamuhitaji mwenzie ili kutekeleza majukumu yake kiufanisi.