Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Uteuzi
Sep 26, 2021
Na Jacquiline Mrisho

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:-(1) Amemteua Bw. Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO. 

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Issa alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Miradi (PDB).(2) Amemteua Bw. Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO.

Kabla ya uteuzi huu, Bw. Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi wa Multichoice Afrika.

Bw. Chande anachukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka.(3) Amemteua Bw. Michael Minja kuwa Kamishna wa Petrol na Gesi, Wizara ya Nishati.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Minja alikuwa mkurugenzi Mkuu – TIPPER.(4) Amemteua Bw. Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu.

Kabla ya uteuzi huu Bw. Mramba alikuwa Mshauri Mkuu wa Kiufundi (Chief Technical Advisor) – TANESCO training School(5) Amemteua Bw. Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Kabla ya uteuzi huu Bw. Seif alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO.

Bw. Said anachukua nafasi ya Bw. Amos Maganga.

Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Septemba, 2021.

Wakati huohuo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga amewahamisha Watumishi Waandamizi watano (5) toka TANESCO kwenda Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambako watapangiwa kazi nyingine kama ifuatavyo:-1. Mhandisi Khalid James – Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji.2. Mhandisi Raymond Seya – Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Masoko.3. Mhandisi Isaac Chanje – Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji.4. Bw. Nyelu Mwamaja – Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi.5. Bw. Amos Ndegi – Mwanasheria wa TANESCO. 

Jaffar Haniu 

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi