Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Utendaji Bora wa Kazi Ndio Utekelezaji Niutakao - Rais Samia
Aug 16, 2023
Utendaji Bora wa Kazi Ndio Utekelezaji Niutakao - Rais Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Mabalozi Wateule pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.
Na Mawazo Kibamba-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaagiza Mabalozi  aliowaapisha wakawajibike ipasavyo ili kuleta tija katika nchi.

Agizo hilo  amelitoa leo  katika hafla ya uapisho wa Mabalozi hao wateule iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Mabalozi Wateule wakila Kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

“Uteuzi wenu huu ni dalili tosha ya imani kubwa ya taifa iliyonayo kwenu ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi nyingine pamoja na taasisi na Jumuiya za kimataifa” amesema Rais Samia.

Mhe. Rais Samia aliendelea kwa  kusisitiza “Nataka mfahamu kwamba dhamana na majukumu mliyopewa ni kubwa na mazito mkaiwakilishe vizuri Tanzania katika nafasi hiyo”.

Aidha, Mhe. Rais Samia amesema Tanzania haiwezi kufanya kazi pekee yake, inahitaji kushirikiana na mataifa mengine kwa kuwa  nayo  yanaihitaji ili kukuza ushirikiano na utengamano katika mambo mbalimbali.

Mabalozi Wateule wakisaini Hati za kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

Kuhusu mahitaji mapya duniani Rais Samia ameyataja baadhi kuwa ni Mabadiliko ya Tabia nchi, Mapinduzi ya Nne ya Viwanda, Matumizi ya Akili  Bandia, Uchumi wa Buluu, Umuhimu wa Madini ya Kimkakati, Utalii Endelevu,


Naye, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Mabalozi wateule kutambua Diplomasia ya nchi  ya kisiasa, kiuchumi pia kibiashara inahitaji kuimarika zaidi hasa wakijua kuwa sera ya nchi ni kuimarisha uchumi wa ndani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili, Jaji Mhe. Sivangilwa Mwangesi kwenye picha ya kumbukumbu na Mabalozi Wateule aliowaapisha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi