Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Upokeaji Mafuta Kupitia Mombasa-Kisumu Hauna Tija: Dkt. Kalemani
Nov 14, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_48865" align="aligncenter" width="807"] Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula (wa nne kutoka kulia) akizungumza jambo wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma Novemba 13, 2019. Wa Pili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua.[/caption]

Na: Veronica Simba na Teresia Mhagama - Dodoma

Wizara ya Nishati imewaambia Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kuwa upokeaji wa mafuta kwa ajili ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani kupitia Mombasa-Kisumu na Ziwa Victoria, hauna tija kwa Taifa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon aliyasema hayo Novemba 13, 2019 jijini Dodoma, wakati wa Semina iliyoandaliwa na Wizara kwa Kamati hiyo.

Alikuwa akiwasilisha mada kuhusu utafiti wa gharama ya upitishaji mafuta kutoka Bandari ya Mombasa – Nairobi – Kisumu hadi Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

[caption id="attachment_48866" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Nishati wakati wa Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma Novemba 13, 2019. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua.[/caption] [caption id="attachment_48867" align="aligncenter" width="807"] Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe hao iliyofanyika jijini Dodoma Novemba 13, 2019 na kuhudhuriwa na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara.[/caption]

Alisema kuwa utafiti huo ulifanywa na timu iliyojumuisha watumishi kutoka Wizara ya Nishati, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na PBPA.

Akifafanua, Mkurugenzi Simon alisema upokeaji mafuta kupitia njia hiyo hauna tija kwa kuzingatia gharama na manufaa kwa nchi, ambazo zinatokana na kutumika kwa bandari za Tanzania.

“Njia ya Mombasa – Kisumu inaweza kuleta athari hasi ukilinganisha na zile chanya. Aidha, miundombinu ya Kanda ya Ziwa na hata ile iliyoko Kisumu, haiwezi kukidhi mahitaji ya Kanda ya Ziwa na nchi za jirani.”

[caption id="attachment_48868" align="aligncenter" width="807"] Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe hao iliyofanyika jijini Dodoma Novemba 13, 2019 na kuhudhuriwa na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara.[/caption] [caption id="attachment_48870" align="aligncenter" width="807"] Baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio, wa tatu kutoka kulia ni, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga na wa nne kutoka kulia ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka.[/caption]

Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa utafiti huo, gharama za usafirishaji kwa njia ya reli ni nafuu kuliko kutumia njia za Mombasa – Kisumu na Dar es Salaam kwa njia ya barabara.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio aliiambia Kamati hiyo kuwa mchango wa sekta ya gesi na mafuta katika uchumi w anchi ni shilingi bilioni 182.05 kati ya mwaka 2005/06 hadi 2015/2016; na  shilingi bilioni 243.05 kati ya mwaka 2016/17 hadi Oktoba 2019.

Aidha, Dkt Mataragio alisema kuwa, matarajio kati ya mwaka 2020/21 hadi 2023/24 ni shilingi bilioni 599.62 na kwamba fedha zilizookolewa kwa kutumia gesi asilia badala ya nishati mbadala kwa matumizi mbalimbali tangu Julai 2004 hadi Oktoba, 2019 ni shilingi trilioni 30.225.

[caption id="attachment_48871" align="aligncenter" width="807"] Kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua wakiwa kwenye Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma Novemba 13, 2019.[/caption]

Akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya gesi asilia katika magari na hatua zinazochukuliwa kwa sasa, Dkt Mataragio alisema Serikali kupitia Wizara ya Nishati, ipo katika hatua za mwisho kukamilisha utafiti wa namna bora ya kusambaza gesi asilia mikoani kwa kutumia mfumo usiotumia mabomba kusafirisha nishati hiyo.

Alisema mradi huo utaanza kutekelezwa katika jiji la Dodoma na baadaye katika mikoa mingine, ambapo utekelezaji wake utawezesha vituo vya kujazia gesi katika magari kuongezeka kwa kasi hivyo kuchochea matumizi ya gesi asilia kama nishati ya kuendeshea magari.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga aliwaambia wajumbe wa Kamati kuwa baada ya miradi mbalimbali ya umeme kukamilika, kumekuwa na mafanikio mengi ikiwemo hali ya upatikanaji umeme vijijini kuongezeka kutoka asilimia mbili mwaka 2007 hadi kufikia asilimia 49.5 mwaka 2016.

[caption id="attachment_48873" align="aligncenter" width="807"] Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio akiwasilisha mada kuhusu masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Taasisi hiyo wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma Novemba 13, 2019.[/caption] [caption id="attachment_48874" align="aligncenter" width="807"] Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon akiwasilisha mada kuhusu masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Taasisi hiyo wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dodoma Novemba 13, 2019.[/caption]

Alisema Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), wanakamilisha utafiti ili kupata takwimu za sasa za upatikanaji umeme nchini hususani vijijini, ambapo alisema takwimu hizo zitapatikana Desemba mwaka huu.

Vilevile alisema kwamba, umeme umefikishwa na kusambazwa katika jumla ya makao makuu ya wilaya 25, ambayo yalikuwa hayajafikiwa na nishati hiyo na kwamba hadi kufikia Oktoba mwaka huu, miundombinu ya umeme imefikishwa kwenye vijiji 8,102 kati ya vijji 12,268 vya Tanzania Bara.

Mada nyingine iliyowasilishwa ni kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sheria ya jotoardhi nchini na uzoefu wa nchi nyingine, ambapo ilielezwa kuwa nishati hiyo ina matumizi mtambuka zaidi ya kuzalisha umeme hivyo huchangia moja kwa moja kwenye sekta nyingine za uchumi zikiwemo za ufugaji, kilimo, viwanda na utalii.

Kuhusu hatua iliyofikiwa katika kudurusu kanuni ya bei za gesi asilia, ilielezwa kuwa, Wizara itakamilisha maboresho ya kanuni kwa kuzingatia maoni chanya ya wadau katika muda mfupi ujao na kwamba kanuni mpya zitazingatia pamoja na mambo mengine, gharama za uwekezaji wa miundombinu ya kuzalisha gesi asilia na usafirishaji.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati, Mwenyekiti wake, Dunstan Kitandula aliishukuru Wizara kwa kuandaa semina hiyo na kwamba itawasaidia kujenga uelewa wa sekta husika ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya kuisimamia.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, aliishukuru Kamati hiyo kwa ushirikiano ambao imekuwa ikitoa kwa Wizara na kuiahidi kuwa, Wizara itaendelea kutekeleza maagizo na miongozo inayotolewa na Kamati husika ili kuhakikisha Watanzania wananufaika kupitia sekta hiyo.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Katibu Mkuu Dkt Hamisi Mwinyimvua, viongozi na wataalamu kutoka wizarani na taasisi zake zote.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi